Tuesday, November 19, 2013

KAGAME, MUSEVENI NA KENYATTA WASHTAKIWA KORTI YA JUMUIYA

kagamepx_deab7.jpg
Serikali za Rwanda, Uganda, Kenya na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, zimefunguliwa kesi katika Mahakama ya Afrika ya Mashariki, zikidaiwa kukiuka mkataba wa kuanzishwa kwa jumuiya hiyo.
Hatua hiyo inatokana na Serikali hizo kufanya vikao vitatu mfululizo na kuzitenga nchi za Tanzania na Burundi.
Walalamikaji katika kesi hiyo, ni Ally Msangi, David Makata na , John Adam, ambao ni Watanzania, wanaotetewa na wakili Mwandamizi, Jimm Obedi wa jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, walalamikaji wamewaomba majaji katika mahakama hiyo, kutoa tamko la kusitisha utekelezaji wa maazimio yote ya vikao vya wakuu wa nchi hizo tatu.
Pia wameomba majaji watoe tamko la kukomesha kurejewa kwa vikao kama hivyo kinyume cha mkataba wa jumuiya hiyo.
Kesi hiyo ya aina yake, ilifunguliwa jana katika Mahakama ya Afrika ya Mashariki na kupokewa na Ofisa Masijala i katika mahakama hiyo, Boniface Ogoti.
Kufunguliwa kwa kesi hiyo, kunakuja siku kadhaa baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzilalamikia nchi hizo, kuhusu kuitenga Tanzania kwa kufanya mikutano mbalimbali ya maendeleo ya nchi zao. Nchi nyingine iliyotengwa ni Burundi.
Kikao cha kwanza cha pamoja kilifanyika Aprili mjini Arusha kabla viongozi hao kukutana Juni 25 na 26 jijini Entebbe nchini Uganda, walidai kuwa na nia moja ya kurahisha mawasiliano katika nchi hizo.
Mkutano mwilingine ulifanyika mjini Kigali Rwanda Oktoba 28 ukiwajumuisha Rais Yoweri Museven wa Uganda, Uhuru Kenyatta (Kenya), Salva Kiir (Sudan Kusini) na Paul Kagame.
Wakili wa walalamikaji Obedi, alisema katika kesi ya msingi, wanawashtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Rwanda, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Uganda,Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Kenya na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo.

DK MVUNGI AZIKWA KIJIJINI KWAO


1461852_10151999781884339_1203660951_n_f818f.jpg
Aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi alizikwa jana kijijini kwake, Chanjale, Kisangara Juu katika mazishi ambayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wajumbe wa tume hiyo, vyama vya siasa na wananchi.
Akizungumza katika mazishi hayo, Askofu Rogath Kimario wa Kanisa Katoliki Dayosisi ya Same alisema tukio la kushambuliwa lililosababisha kifo chake halikuwa la ujambazi.
Akizungumza wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika Kanisa la Moyo Mtakatifu Yesu la Parokia ya Kisangara Juu iliyopo Chanjale, ambayo pia ilihudhuriwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Arusha, Josephat Lebulu; Askofu wa Jimbo la Mbulu, Beatus Kinyaiya na Askofu Damiani Ngalu wa Geita wote wa Kanisa Katoliki, Askofu Kimario alisema waliofanya mauaji hayo ni wauaji wa kimtandao na kuitaka Serikali kutoa majibu sahihi kuhusiana na tukio hilo badala ya majibu mepesi yasiyofanyiwa utafiti.
Kauli hiyo ilionekana kujibu ile ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova kuwa mauaji ya Dk Mvungi ni tukio la ujambazi.

ERNIE BRANDTS KUREJEA NCHINI JUMAPILI

Ernest_5e767.jpg
KOCHA Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts anatarajiwa kutua nchini Jumapili Novemba 24 kusaini mkataba mpya wa kuitumikia timu hiyo katika mzunguko wa pili.
Brandts amemaliza mkataba wa kuitumikia timu hiyo katika mzunguko wa kwanza ambapo kwa sasa wapo kwenye mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo kwa ajili ya kuingia mkataba mpya.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah Bin Kleb alisema, wameshamalizana na kocha hivyo wanasubili akitua tu nchini Novemba 24 ndio wamsainishe mkataba mpya.

"Brandts anatarajia kutua nchini Novema 24 ambapo ndipo likizo yake itakuwa imefikia tamati kwa ajili ya kuja kukiandaa kikosi kwa ajili ya mzunguko wa pili.
"Mara tu atakapotua ndio tunaingianae mkataba mpya, hadi sasa hatujajua tutamsainisha wa muda gani lakini usiozidi chini ya mwaka mmoja," alisema Bin Kleb.

Sunday, November 17, 2013

TAIFA STARS SASA KUIKABILI ZIMBABWE J4


Taifa Stars sasa inacheza na Zimbabwe mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date itakayofanyika keshokutwa Jumanne (Novemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Awali Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilikuwa icheze na Kenya (Harambee Stars), lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF) lilituma taarifa jana jioni (Novemba 16 mwaka huu) likieleza kuwa timu yake haitacheza tena mechi hiyo.

Kikosi cha Zimbabwe chenye msafara wa watu 30 kinatarajia kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kesho (saa 3 asubuhi) tayari kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 11 kamili jioni.

NIGERIA YA KWANZA KUKATA TIKETI YA BRAZIL 2014 BAADA YA KUIFUMUA ETHIOPIA 2-0

article-2508386-1973888200000578-737_634x423_5ac75.jpg
Timu ya taifa ya Nigeria imekua nchi ya kwanza ya Afrika kukata tiketi ya kecheza. Fainali za Kombe la Dunia mwakani baada ya ushindi wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Ethiopia leo. Victor Moses alifunga kwa penalti dakika ya 20 na Victor Obinna akaongeza la pili dakika ya 82 kwa mpira wa adhabu, hivyo Super Eagles kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 4-1, baada ya awali kushinda 2- mjini Addis Ababa mwezi uliopita katika mchezo wa kwanza

IVORY COAST NAYO YAFUZU KOMBE LA DUNIA BAADA YA SARE YA1-1 NA SENEGAL

IvoryCoast-celebrates130122G300_2ccf2.jpg
TIMU ya taifa ya Ivory Coast imefuzu Fainali zijazo za Kombe la Dunia baada ya sare ya 1-1 usiku huu ugenini na Senegal kwenye Uwanja wa Mohamed V in Casablanca, Morocco.
Matokeo hayo yanaifanya Didier Drogba na wenzake wafuzu kwa ushindi wa jumla wa 4-2 na kuungana na Nigeria iliyoitoa kwa jumla ya mabao 4-1 Ethiopia.
Ikiwa inajivunia ushindi wa 3-1 katika mchezo wa kwanza, Tembo walilazimika kusota kusawazisha bao baada ya Moussa Sow kutangulia kuwafungia Simba wa Teranga kwa penalti, kabla ya Salomon Kalou kusawazisha dakika za majeruhi.
Kikosi cha Senegal: Coundoul, S. Sane, L. Sane, Mane, Badji/Saivet dk82, P. Cisse, Mbodji, Gueye, Souare, Djilobodji na Ndoye/Sow 66.
Ivory Coast: Barry, K. Toure, Bamba, Gosso, Zokora, Romaric, Aurier, Y. Toure, Kalou, Gervinho/Sio dk80 na Drogba

Wednesday, October 30, 2013

WANAJESHI WALIOIBA VITU WESTGATE WAKATI WANAPAMBANA NA MAGAIDI WAFUKUZWA KAZI NA KUFUNGWA

Nairobi, Kenya. Wanajeshi wawili nchini Kenya wamefutwa kazi na kufungwa jela kwa kitendo cha kupora mali wakati wa shambulizi la kigaidi kwenye Jengo la Westgate mwezi jana.  Hayo yamesemwa na mkuu wa jeshi la Kenya, Julius Karangi.

Karangi amesema kuwa mwanajeshi wa tatu aliyeshukiwa kwa uporaji anachunguzwa.

Awali Karangi alikanusha kuwa wanajeshi walifanya uporaji kwenye jengo hilo licha ya picha za CCT kuonyesha wanajeshi wakibeba mifuko ya plastiki kutoka kwenye moja ya maduka makubwa yaliyokuwa ndani ya Jengo la Westgate.

WEMA SEPETU AFUNGUKA JINSI BABA YAKE ALIVYOTESEKA MPAKA MAUTI ILIPOMCHUKUA

Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu akielezea kuhusu msiba wa baba yake mzazi Balozi Abraham Isaac Sepetu alipoongea na GLOBAL TV. Balozi Sepetu alifariki asubuhi ya Jumapili Oktoba 27, 2013 katika hospitali ya TMJ jijini Dar na mwili wake jana nyumbani kwake Sinza-Mori jijini Dar es Salaam tayari kwa mazishi yatakayofanyika leoVisiwani Zanzibar.

Wednesday, October 16, 2013

KUMBE SHOW ZA MAJUU SIO KAMA ZA BONGO! - OMMY DIMPOZ


Ommy alikuwa akiongea na kipindi cha Ampilifaya jana baada ya kurejea kutoka nchini Marekani alikokuwa kwenye ziara ya wiki tatu.

“Naweza kusema hapa nyumbani tunalipwa hela nyingi kuliko tunavyopata nje kwa msanii yeyote kwa asilimia kubwa. Inategemea pia unaenda kufanya tamasha sehemu gani. Kwahiyo asilimia kubwa hela unatengeneza zaidi nyumbani,”alisema Ommy.

Alisema hiyo ni kwasababu show za Tanzania huhudhuriwa na watu wengi zaidi kuliko inavyokuwa nchi za nje ambako ni watu wachache sana huingia japo kiingilio ni kikubwa na wengi wanaohudhuria ni watu waliotoka Afrika Mashariki zaidi.
Katika hatua nyingine, leo Ommy Dimpoz kupitia Instagram, ameandika maneno ya shukrani kwa wote walioifanikisha show yake.

“AssaLaam ALeykum Ndugu zangu, Eid MubaraQ Ndugu, jamaa, Marafiki, and all my Fans all over the world…Namshukuru Mungu Alhamdulilah nimerudi nyumbani Salama Kuendelea na Majukumu mengine baada ya Tour ya Takriban Mwezi Mmoja…Ningependa kuchukua Nafasi hii kuwashukuru @Dmkglobal promotion na J&P kwa kufanikisha tour yangu ambayo imeweza kuwa na Mafanikio makubwa Na kufanikisha baadhi ya malengo ambayo mengine sikuyatarajia.
Pia ningependa kuwashukuru watu wote ambao walionyesha support kipindi chote cha tour yangu hususan Watanzania wenzangu na Watu wa Africa Mashariki na Kati ambao walionyesha Ushirikiano na support ya kutosha tangia mwanzo mpaka mwisho wa tour yangu…Nachoweza kuwaahidi ni kuwa mengi mazuri Yanakuja na Naimani sitawaangusha.Nawatakia mapumziko na sherehe njema za sikukuu ya Idd…. Mimi na team nzima ya pozkwapoz tutakuwa DARLIVE tukitoa Huduma Karibuni sana. LOVE U ALL.” na Vijimambo Blog

MAGAZETI YA LEO JUMATANO OKTOBA 16, 2013

DSC 0137 46fbc
DSC 0138 47cac

KENY PINO BLOG NA JAMBO TZ BLOG WANAWATAKIA EID MUBARAK NYOTE!


Monday, October 14, 2013

ZITTO KABWE:SHILINGI BILIONI 67.7 ZIMELIPWA NA SERIKALI KWA VYAMA VYA SIASA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 4, 2009/2010 MPAKA 2012/2013



Shilingi bilioni 67.7 zimelipwa na Serikali kwa vyama vya siasa katika kipindi cha miaka 4, 2009/2010 mpaka 2012/2013. Fedha hizi hazijakaguliwa kwa mujibu wa Sheria. 

Mahesabu ya Vyama vya siasa nchini yanapaswa kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali kwa mujibu wa Sheria tangu mwaka 2009. Tangu mwaka huo Kamati ya PAC haijawahi kuona Taarifa ya CAG kuhusu ukaguzi wa vyama vya siasa. 

Kamati imemwita Msajili wa vyama ili kufafanua ni kwa nini Vyama vya Siasa nchini havifuati sheria (vifungu vya sheria vimeambatanishwa hapa chini). Uvunjifu huu wa Sheria ni wa makusudi au wa kutokujua? Sheria inataka Mahesabu ya vyama yatangazwe kwa uwazi, tena kwa Government Notice. Umewahi kuona?

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAONGOZA WATANZANIA KATIKA SHEREHE ZA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2013

Picha no 2Rais Jakaya Kikwete akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2013 Bw.Juma Ali Simai leo katika uwanja wa CCM Samora mjini Iringa.Picha na 1Vijana wa Halaiki wakitoa burudani kwa kuimba nyimbo mbalimbali zinazohamasisha umoja wa taifa leo wakati wa kilele cha mbio za mwenge wa uhuru katika viwanja vya Samora mjini Iringa. Picha na 3Wakimbiza Mwenge wa Uhuru 2013 wakiingia katika viwanja vya CCM Samora mkoani Iringa leo. Picha na 4 Kiongozi wa mbi za Mwenge wa Uhuru 2013 Bw. Juma Ali Simai akisoma risala ya ujumbe wa wananchi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete leo mjini Iringa. Picha na 5 Rais Jakaya Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakimbiza mwenge wa Uhuru 2013 leo mjini Iringa.
Picha na 6 Rais Jakaya Kikwete na mama Salma Kikwete (wa tatu kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiongozwa na Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Fenella Mukangara (wa nne kutoka kushoto)
Picha na 7Wananchi wa mkoa wa Iringa na vijana wa halaiki wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa Kilele cha mbio za Mwenge leo mkoani Iringa.

Wednesday, September 25, 2013

ANGALIA VIDEO IKIONYESHA JINSI FAMILIA HII ILIVYO OKOLEWA KUTOKA NDANI YA JENGO LA WESTGATE-SAD



We’ve all seen this iconic photo of this mother and her two young children laying down calmly as the attack went on on Nairobi’s Westgate mall. Here is a short video showing them being evacuated to safety. Notice the little girl did not let go of her freshly bought Bata paper bag containing her new pair of shoes.
it is so sad that the children actually knew they had to lie still, even the little boy must have known that something is terribly wrong, so he didnt move even a bit... it just makes me so sad.. children never should have experience such bad things

 Video: Exclusive Footage of The Rescue Of Mother & Her Children #WestgateMall

AL SHABAAB NI NANI...???

00 a9dd3
ULIMWENGU umepatwa na mshtuko mkubwa kwa kuona picha za tukio kubwa la kigaidi kwenye moja ya maduka makubwa jijini Nairobi. Hili ni shambulio kubwa la kigaidi kupata kutokea Afrika Mashariki tangu lile la mwaka 1998. Na ajabu ya kihitoria ni kuwa matukio mengi ya kigaidi yametokea katika mwezi wa Septemba.
La Nairobi ni shambulizi la kigaidi la kulaaniwa vikali na wapenda amani wote ulimwenguni. Hata hivyo, moja ya tafsiri ya vitendo vya kigaidi tunavyovishuhudia Nairobi ni kuwepo kwa hali ya vita vya kigaidi vyenye kuendeshwa kwenye maeneo ya mijini (Urban terrorism).
Ni shambulizi lenye athari mbaya kiuchumi si tu kwa nchi ya Kenya, bali hata majirani zake ikiwemo Tanzania. Ni shambulizi lililowaogopesha wageni wengi wakiwamo wawekezaji pia. Kwamba Al Shabaab inalenga pia nchi za Magharibi. Hivyo basi,
hata raia wake. Kunahitajika jitihada za pamoja kuwaondoa hofu watu wa mataifa ya nje, kuwa kilichotokea Nairobi kitadhibitiwa kwa njia zote, kisitokee tena.

SIMULIZI MBALI MBALI ZA KUTISHA KUTOKA MAUJI YA WESTGATE NAIROBI


MJAMZITO wa miezi nane na nusu ni miongoni mwa mateka waliouawa katika uvamizi wa kituo cha biashara cha Westgate jijini Nairobi Jumamosi, imefahamika.

Elif Yavuz ambaye ni msomi wa Chuo Kikuu cha Havard, Marekani aliuawa pamoja na mumewe Ross Langdon (33) ambaye ni msanifu majengo mwenye uraia pacha wa Uingereza na Australia.

Taarifa zilizopatikana jana kutoka eneo la tukio zilisema Langdon ameshiriki miradi mbalimbali barani Afrika, ikiwamo inayohusika na ujenzi upya wa hospitali ya Ukimwi nchini Kenya bila malipo yoyote.

Elif ambaye alikuwa akitarajiwa kujifungua wiki mbili zijazo, aliuawa sambamba na mumewe huyo ambaye alipata kuwa mshindi wa tuzo ya ujenzi.

Langdon alipata mafunzo ya ujenzi katika Chuo Kikuu cha Tasmania kisha Chuo Kikuu cha Sydney, na kufanya kazi katika kampuni kadhaa kabla ya kuanzisha Kampuni yake ya Regional Associates Ltd, Mei 2008.

Akizaliwa na kukulia Kusini Mashariki mwa Tasmania, miongoni mwa miradi aliyoshiriki iko Uganda, Rwanda na Tanzania.

Alikuwa mtaalamu wa masuala ya malaria akifanya kazi Kenya katika Wakfu wa Bill, Hillary and Chelsea, ulioanzishwa na Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton, Yafuz pia alipata kufanya kazi na Wakfu wa Bill and Melinda Gates unaoendeshwa na bilionea muasisi wa Microsoft, Bill Gates.

Akizaliwa Uholanzi, Yavuz ameishi Cambridge, Massachusetts, wakati akisoma Chuo Kikuu maarufu duniani cha Havard. Esther Waters-Crane, mtaalamu wa Uingereza ambaye anamfahamu vizuri Elif, alielezea masikitiko yake kwa kumpoteza mama huyo mtarajiwa na jinsi Kenya ilivyoshughulikia shambulizi hilo lisilo na sababu.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 25, 2013

DSC 0027 aa995
DSC 0028 f54fc

Friday, September 20, 2013

SWANSEA YAICHAPA VALENCIA 3-0 EUROPA LEAGUE

toten2 982a3
Swansea wakishangilia bao
WAKALI wa soka ya kitabuni England, Swansea wameanza vyema Europa League baada ya kuifumua mabao 3-0 nyumbani kwake Valencia iliyomaliza na wachezaji 10.
Wenyeji walilazimika kucheza 10 kwa takriban dakika 80, baada ya beki Adil Rami kutolewa nje kwa kadi nyekundu, kufuatia kumchezea rafu Wilfried Bony.
Mshambuliaji huyo ndiye aliyeifungia Swansea bao la kwanza dakika ya 14 usiku huu, hilo likiwa bao lake la tano katika mechi nanemsimu huu.
Mabao mengine yalifungwa na Michu dakika ya 58 na Jonathan de Guzman dakika ya 62.
Kikosi cha Valencia kilikuwa: Guaita, Barragan, Rami, Feghouli/Pabon dk59, Mathieu, Ever/Costa dk14, Javi Fuego, Guardado, Canales/Bernat dk66, Cartabia na Postiga.
Swansea: Vorm, Rangel/Davies dk56, Amat, Chico, Tiendalli, de Guzman, Canas, Pozuelo, Dyer/Lamah dk65, Michu/Shelvey dk77 na Bony.
Katika mchezo mwingine, mabao mawili ya Jermain Defoe yalichgia ushindi wa 3-0 kwa Tottenham dhidi ya Tromso, bao lingine akifunga Christian Eriksen.
toten 7d48c
Pamoja na ushindi huo, Mousa Dembele, Danny Rose and Younes Kaboul wote walitoewa nje baada ya kuumia.
Tottenham ilimaliza mechi na wachezaji 10 kutokana na Kaboul kutolewa nje baada ya kuumia, wakati kocha Andre Villas-Boas amemaliza idadi ya wachezaji wa kubadili.
Spurs: Lloris, Naughton, Kaboul, Dawson, Rose, Sandro, Dembele, Sigurdsson, Holtby, Lamela na Defoe.
Tromso: Sahlman, Kristiansen, Fojut, Koppinen, Causevic, Bendiksen, Johansen, Drage, Pritchard, Moldskred, Ondrasek. Chanzo: binzubeiry

MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 20, 2013

DSC 0032 8b966
DSC 0033 c2442
DSC 0034 af156

MNIGERIA ASHINDA SHINDANO LA UREMBO LA KIISILAMU

mrembo 25c93 Mwanadada wa Nigeria ndiye mshindi wa shindano la urembo kwa wasichana wa kiisilamu mjini Jakarta Indonesia.




Obabiyi Aishah Ajibola, 21, alishinda shindano la kimataifa la wasichana wa kiisilamu kwa jina Muslimah mwaka 2013 siku ya Jumatano.

Washindani 20 walishiriki mashindano hayo kuonyesha mitindo ya kiisilamu pamoja na maadili ya kiisilamu wakati wa mashindano hayo.

Mashindano yalifanyika kabla ya shindano kubwa zaidi la mwanamke mrembo zaidi duniani, ambalo limeghadhabisha makundi ya watu wenye msimamo mkali nchini Indonesaia kwa kutaka kuandaliwa huko.

JESHI LA POLISI LAPIGA MARUFUKU MAANDAMANO YA F, CHADEMA NA NCCR HAPO JUMAMOSI


Jeshi la Polisi Jijini Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano ya umoja wa vyama vya CUF, NCCR na CHADEMA siku ya Jumamosi yaliyokuwa yamepangwa  kuanzia Tazara hadi Jangwani na Mwenge hadi Jangwani na sehemu mbalimbali ...

Taarifa  iliyotolewa  na kamanda Kova  kupitia  ITV   imeeleza  kuwa  Polisi wamechunguza na kugundua kwamba  maandamano  hayo  yataleta usumbufu kwa watu wengine na kwamba kwa kuwa lengo ni kufika Jangwani basi Viongozi wa vyama hivyo wawaambie wafuasi wao waende Jangwani bila Maandamano.

Source: ITV HABARI SAA 2 usiku

MILIONI 58 ZAPATIKANA mechi SIMBA SC, MGAMBO TANGA

Boniface-Wambura1 655d3
MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Simba SC na Mgambo Shooting Stars iliyochezwa jana (Septemba 18 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam umeingiza Sh. 58,365,000.

Watazamaji 10,241 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 23 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa wenyeji Simba kuibuka na ushindi wa mabao 6-0.

Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 13,839,327.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 8,903,135.59.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,036,946.16, tiketi sh. 2,548,890, gharama za mechi sh. 4,222,167.70, Kamati ya Ligi sh.
4,222,167.70, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,111,083.85 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,641,954.10.

Wakati huo huo; Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa siku 14 kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na za Ligi ya Daraja la Kwanza (FDL) kuwasilisha mikataba ya makocha wao.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana Septemba 12 mwaka huu imebaini klabu nyingi hazijawasilisha mikataba ya mabenchi yao ya ufundi, kitu ambacho ni matakwa ya kikanuni. Siku hizo 14 zimetolewa kuanzia Septemba 17 mwaka huu.

Kwa klabu ambazo zitashindwa kuwasilisha mikataba hiyo na vielelezo vingine ndani ya mudau huo zitachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni. Chanzo: TFF

SITTA AWATETEA WAHAMAJI HARAMU...!!!


Ataka operesheni ifanywe kibinaadamu

• Ahoji kama Watanzania nao watafukuzwa itakuaje

Na Fatuma Kitima,DSM

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, ametoa wito kwa mamlaka zinazohusika katika operesheni ya kuwasaka wahamiaji haramu kutumia ubinadamu zaidi katika utelezaji wa zoezi hilo.

Hayo yalisemwa jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Sitta alikiri kuna mapungufu katika zoezi hilo na kusema amri ya rais inatakiwa kutekelezwa lakini kwa kuzingatia haki za binaadamu.

ICC YATAKA MAREKANI IMKAMATE RAIS BASHIR

al-bashir_bcdb9.jpg
Siku mbili baada ya Rais wa Sudan kuiomba Marekani kumpa Visa ya kusafiri nchini humo kuhudhuria mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, wito umetolewa kwa taifa hilo kumkamata Bashir na kumkamabidhi kwa mahakama ya ICC.
Mkutano huo utafanyika wiki ijayo.
Ombi hilo limetolewa na ICC kwa Marekani na kuitaka impe Visa Bashir na kisha kumkamata na kumkabidhi kwa mahakama hiyo pindi tu atakapotua nchini humo.
Bashir anatakikana na mahakama ya ICC kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu na pia kuamuru mauaji ya halaiki katika jimbo la Darfur.
Marekani ilisema kuwa ilipokea ombi la Bashir kutaka Visa na kulitaja ombi hilo kama la kuudhi na kejeli kubwa kwa taifa hilo. Ilimtaka Bashir kwanza kujikabidhi kwa mahakamya ICC kabla ya kutaka kuingia Marekani.
Hata hivyo Marekani sio mwanachama wa mahakama ya ICC na kwa hivyo , kisheria sio lazima itimize matakwa ya mahakama hiyo juu ya Bashir.
Marekani imekuwa katika msitari wa mbele kutaka Bashir akamatwe kwa madai ya uhalifu dhidi yake ili akabiliwa na sheria za kimataifa
Shirika la habari la Reuters lilisema kua mahakama imeshauri Marekani kumkamata Bashir na kumkabidhi kwa ICC ikiwa ataingia nchini humo.
Vibali viwili vya kumkamata Bashir vilitolewa mwaka 2009 na 2010 kwa madai ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Hata hivyo Sudan imepuuza hatua ya ICC kumtaka Bashir kwa makosa ya Darfur wakisema kuwa madai hayo yameongezwa chumvi, na nchi hiyo imekataa kuitambua mahakama hiyo ikisema kuwa ni sehemu ya njama ya nchi za magharibi dhidi ya Afrika.

RAIS KIKWETE AWASHUKIA WANASIASA

 
Rais Jakaya Kikwete
 
*Asema hatawatetea wauza ‘unga’
*Ashangazwa na kiwango cha uongo

RAIS Jakaya Kikwete, amesema anashangazwa na kiwango cha uongo cha baadhi ya wanasiasa ambao hakuwataja majina, kuwa wamekuwa wakizusha madai kuwa Rais aliteua wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, bila kuongozwa na mapendekezo ya wadau mbalimbali waliopendekeza majina hayo.
Alisema bado anaendelea kuamini mchakato wa Katiba mpya utafikia mwisho wake mwaka 2014 na hivyo kuiwezesha Tanzania kufanya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, chini ya Katiba mpya.

Alisema hana tatizo na watu wanaopinga sera za serikali ama hata kumpinga yeye binafsi, bali tatizo lake ni wanasiasa na wanaharakati wanaochochea ghasia, fujo na uvunjifu wa amani.

Rais Kikwete, aliyasema hayo juzi, mjini San Rafael, California, nchini Marekani, wakati alipokutana na kuzungumza na jumuia ya Watanzania waishio katika Jimbo la California.

Katika hotuba yake, ambayo alizungumzia mambo mbalimbali, Rais Kikwete aligusia mjadala wa karibuni bungeni kuhusu mchakato wa Katiba mpya na kusema kuwa alishangazwa na madai kuwa yeye kama Rais, hakuongozwa na mapendekezo ya wadau wakati anateua Tume ya Katiba.

NAPE AWACHONGANISHA CHADEMA NA WAKULIMA WA PAMBA


blog_756b7.jpg
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa wilaya ya Bariadi kwenye Viwanja vya Sabasaba. Adai wamechukizwa na viwanda vya nguo,nyuzi ,nyama na ajira. -Asema misaada ya China ni ukombozi mkubwa unaowakera Chadema. -Awataka kanda ya ziwa kuujua unafiki huo wa Chadema.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya Chadema kukerwa na hatua za Balozi wa China na serikali ya China kwa ujumla katika kushiriki katika hatua za kuwakwamua watanzania katika umasikini.

Nape alisema hayo jana alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mji wa Bariadi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya CCM sabasaba Mkoani Simiyu.

Tuesday, September 17, 2013

WATUHUMIWA WA MAUAJI YA BILIONEA ERASTO MSUYA WAKUTWA KWA SANGOMA

Jeshi la polisi mkoa wa kilimanjaro linawashikilia watu wanne zaidi wakidaiwa kuhusika na mauaji ya mfanyabiashara bilionea wa madini ya tanzanite Arusha Erasto Msuya 43 wawili kati yao walikutwa kwa mganga wa kienyeji (sangoma) wakifanyiwa zindiko ili wasikamatwe na vyombo vya dola.

Pia jeshi limenikiwa kunasa bunduki aina ya SMG yenye namba za usajili KJ10520,inayoaminika kutumika katika mauaji hayo.Msuya aliuawa kwa kupingwa risasi zaidi ya 10 kifuani Augost 7mwaka huu,katika eneo la mijohoroni wilayani Hai.

Akizungumza na waandishi wa habari jana,kamanda wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Robert Boaz aliwataja watuhumiwa kuwa ni Sadiki Jabiri 32 mkazi wa Dar es Salaam na Lang'angata wilayani Hai .

MWALIMU AKAMATWA AKIWAFANYIA WANAFUNZI MTIHANI WA DARASA LA SABA IRINGA

Jeshi la  polisi  mkoani Iringa  linamshikilia mwalimu wa  shule ya msingi Makungu wilaya ya  Mufindi Bw Edwin Ambukile kwa  tuhuma  za  kuwasaidia majibu wanafunzi wa  darasa la  saba katika mtihani  wa Taifa  wa kuhitimu elimu ya msingi.
Kamanda  wa polisi mkoa  wa Iringa Bw Ramadhan Mungi amesema  kuwa tukio  hilo limetokea  Septemba 15 mwaka  huu  .
Alisema kuwa mwalimu  huyo ambae ni mwalimu wa masomo ya Sayansi katika  shule  hiyo pia alikuwa ni mwalimu wa masomo ya ziada ( katika  shule  hiyo na  sababu ya  kuwasaidia  wanafunzi majibu ni kutaka  kupata umaarufu kwa wanafunzi  watano aliokuwa akiwafundisha masomo ya  ziada aliopata  kuwaahidi kuwa watafaulu mtihani  huo.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE SEPTEMBA 17, 2013

DSC 0094 87348
DSC 0095 5e40c

KINANA AMPONZA BALOZI WA CHINA... CHADEMA KUMSHITAKI KWENYE MAHAKAMA YA KIMATAIFA

http://3.bp.blogspot.com/-tB-YS2RGEHk/UjfrTKmUq2I/AAAAAAAAl3k/wO2eYdRF-0M/s1600/1.png
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kitamshitaki Balozi wa China nchini, Lu Younqing Umoja wa Mataifa (UN) kwa kukiuka Mkataba wa Vienna (Vienna Convention) wa mwaka 1964 ambao unaeleza uhusiano wa kibalozi kati ya nchi na nchi.


Aidha, kimesema kitaiandikia barua Serikali ya China ili kutaka ufafanuzi kama imemtuma Balozi wake kufanya kazi ya uenezi siasa kwenye vyama.


Tukio la Balozi huyo kuhudhuria mkutano wa hadhara wa CCM lilitokea Septemba tisa mwaka huu kwenye mkutano wa chama hicho uliofanyika Wilaya ya Kishapu Shinyanga, ambapo Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana alimtambushisha balozi huyo huku akiwa amevaa sare za chama hicho.

WAMALAWI WAMIMINIKA KATIKA OFISI ZA UHAMIAJI JIJINI DAR KWAAJILI YA KUJIORODHESHA UHALALI WA KUISHI TANZANIA

Raia wa Malawi wakiwa katika foleni ya kuingia kujiandikisha katika Idara ya Uhamiaji, Mkoa wa Dar es Salaam jana kuhusu zoezi linaloendelea la kuwatambua wahamiaji haramu jijini Dar es Salaam. Mamia ya wakazi hao walimiminia katika ofisi hizo leo kujiorodhesha ikiwa ni agizo la Rais Jakaya Kikwete.
Akina mama na watoto wakisubiri kujiorodhesha.
Ofisa wa Uhamiaji akiwaelekeza jambo Raia wa Malawi. Credits: Father Kidevu Blog

Saturday, September 14, 2013

IPIGIE KURA BLOG YAKO YA JAMBO TZ ILI IWEZE KUSHINDA KATIKA TANZANIA BLOGS AWARDS

 
Upigaji kura umeanza (7/09/2013), blog hii imeshiriki kipengele cha The Best Newcomer Blog

Jinsi ya kuPiga kura, gonga/bofya/ click hayo maandishi yaliyoandikwa piga kura yako hapa, kisha chagua jambotz8.blogspot.com malizia na vote now.

 PIGA kura yako hapa..........!!! Jambo Tz

Ahsante Kwa Kutupigia Kura.

PADRI AMWAGIWA TINDIKALI ZANZABAR

padri_2e446.png
Polisi huko visiwani Zanzibar wanachunguza tukio la kasisi wa kanisa katoliki kushambuliwa kwa tindikali.
Imeelezwa kuwa Kasisi huyo Anselmo Mwang'amba, alimwagiwa tindikali akitoka mgahawa mmoja wa kutumia mtandao mjini Zanzibar. Tukio hilo linatokea ndani ya mwezi mmoja tangu wasichana wawili wa kiingereza kushambuliwa.
Hili ni janga jingine kwa Zanzibar ambayo imekuwa ikizongwa na matukio ya aina hii kwa muda sasa.
Mkurugenzi wa upelelezi wa Zanzibar, Yusufu Ilembo ameieleza BBC kuwa bado hawajakamata mtu yoyote kuhusika na tukio hilo ingawa amethibitisha kuwa uchunguzi tayari umeanza.
Ameeleza kuwa Kasisi Mwang'amba aliungua usoni na mabegani na kwamba anaendelea kutibiwa.  Tembelea jambotz8.blogspot.com kila siku.
Katika miaka ya karibuni Zanzibar imekabiliwa na mikasa ya watu kushambuliwa hivi na kuzua hisia kuwa chuki za kidini.
Mapema mwaka huu kasisi mwingine wa kanisa katoliki alishambuliwa kwa risasi na kuuawa.
Mwezi uliopita Zanzibar ilitikisika kutokana na wasichana wawili wangereza kushambuliwa kwa tindikali na watu wasiojulikana.
Kiongozi mmoja wa dini ya kiislamu pia alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 14, 2013

DSC 0020 3186e
DSC 0021 4ba64

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...