Ataka operesheni ifanywe kibinaadamu
• Ahoji kama Watanzania nao watafukuzwa itakuaje
Na Fatuma Kitima,DSM
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Samwel Sitta, ametoa wito kwa mamlaka zinazohusika katika
operesheni ya kuwasaka wahamiaji haramu kutumia ubinadamu zaidi katika
utelezaji wa zoezi hilo.
Hayo yalisemwa jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Sitta alikiri kuna mapungufu katika
zoezi hilo na kusema amri ya rais inatakiwa kutekelezwa lakini kwa
kuzingatia haki za binaadamu.
Alisisitiza kuwa ubinadamu utumike kwa kuwa baadhi ya wahamiaji hao, wana familia na wamewekeza nchini kwa muda mrefu.
“Baadhi yao wana familia, mali zao sasa endapo atachukuliwa tu ataenda wapi,” alihoji.
Alisema suala hilo linahitaji kufikiriwa
kwa kina na kuhoji jee itakuwa vizuri kama Watanzania wanaoishi
mipakani mwa nchi jirani nao watafukuzwa.
Kuhusu Tanzania kutoshirikishwa katika
mikutano ya wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Sitta alisema nchi
hizo zina haki ya kufanya mikutano na kushirikiana katika baadhi ya
mambo kwa mujibu wa mkataba iwapo nchi moja itakuwa haijawa tayari
kushiriki lakini akasema wanachoomba ni ushirikishwaji.
Alisema kwa sasa Tanzania haijakubaliana
na nchi nyengine wanachama wa Afrika Mashariki kuwa ifikapo Oktoba 15
rasimu ya shirikisho iwe tayari jambo ambalo haliwezekani kwa haraka
kwakuwa bado kuna mambo matatu hayajatelezeka katika makubaliano.
Aliyataja mambo hayo ni makubaliano ya ushuru wa pamoja, soko la pamoja na mfumo wa sarafu moja.
No comments:
Post a Comment