Shilingi
bilioni 67.7 zimelipwa na Serikali kwa vyama vya siasa katika kipindi
cha miaka 4, 2009/2010 mpaka 2012/2013. Fedha hizi hazijakaguliwa kwa
mujibu wa Sheria.
Mahesabu
ya Vyama vya siasa nchini yanapaswa kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Mahesabu ya Serikali kwa mujibu wa Sheria tangu mwaka 2009.
Tangu mwaka huo Kamati ya PAC haijawahi kuona Taarifa ya CAG kuhusu
ukaguzi wa vyama vya siasa.
Kamati
imemwita Msajili wa vyama ili kufafanua ni kwa nini Vyama vya Siasa
nchini havifuati sheria (vifungu vya sheria vimeambatanishwa hapa
chini). Uvunjifu huu wa Sheria ni wa makusudi au wa kutokujua? Sheria
inataka Mahesabu ya vyama yatangazwe kwa uwazi, tena kwa Government
Notice. Umewahi kuona?