Friday, September 20, 2013

SWANSEA YAICHAPA VALENCIA 3-0 EUROPA LEAGUE

toten2 982a3
Swansea wakishangilia bao
WAKALI wa soka ya kitabuni England, Swansea wameanza vyema Europa League baada ya kuifumua mabao 3-0 nyumbani kwake Valencia iliyomaliza na wachezaji 10.
Wenyeji walilazimika kucheza 10 kwa takriban dakika 80, baada ya beki Adil Rami kutolewa nje kwa kadi nyekundu, kufuatia kumchezea rafu Wilfried Bony.
Mshambuliaji huyo ndiye aliyeifungia Swansea bao la kwanza dakika ya 14 usiku huu, hilo likiwa bao lake la tano katika mechi nanemsimu huu.
Mabao mengine yalifungwa na Michu dakika ya 58 na Jonathan de Guzman dakika ya 62.
Kikosi cha Valencia kilikuwa: Guaita, Barragan, Rami, Feghouli/Pabon dk59, Mathieu, Ever/Costa dk14, Javi Fuego, Guardado, Canales/Bernat dk66, Cartabia na Postiga.
Swansea: Vorm, Rangel/Davies dk56, Amat, Chico, Tiendalli, de Guzman, Canas, Pozuelo, Dyer/Lamah dk65, Michu/Shelvey dk77 na Bony.
Katika mchezo mwingine, mabao mawili ya Jermain Defoe yalichgia ushindi wa 3-0 kwa Tottenham dhidi ya Tromso, bao lingine akifunga Christian Eriksen.
toten 7d48c
Pamoja na ushindi huo, Mousa Dembele, Danny Rose and Younes Kaboul wote walitoewa nje baada ya kuumia.
Tottenham ilimaliza mechi na wachezaji 10 kutokana na Kaboul kutolewa nje baada ya kuumia, wakati kocha Andre Villas-Boas amemaliza idadi ya wachezaji wa kubadili.
Spurs: Lloris, Naughton, Kaboul, Dawson, Rose, Sandro, Dembele, Sigurdsson, Holtby, Lamela na Defoe.
Tromso: Sahlman, Kristiansen, Fojut, Koppinen, Causevic, Bendiksen, Johansen, Drage, Pritchard, Moldskred, Ondrasek. Chanzo: binzubeiry

MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 20, 2013

DSC 0032 8b966
DSC 0033 c2442
DSC 0034 af156

MNIGERIA ASHINDA SHINDANO LA UREMBO LA KIISILAMU

mrembo 25c93 Mwanadada wa Nigeria ndiye mshindi wa shindano la urembo kwa wasichana wa kiisilamu mjini Jakarta Indonesia.




Obabiyi Aishah Ajibola, 21, alishinda shindano la kimataifa la wasichana wa kiisilamu kwa jina Muslimah mwaka 2013 siku ya Jumatano.

Washindani 20 walishiriki mashindano hayo kuonyesha mitindo ya kiisilamu pamoja na maadili ya kiisilamu wakati wa mashindano hayo.

Mashindano yalifanyika kabla ya shindano kubwa zaidi la mwanamke mrembo zaidi duniani, ambalo limeghadhabisha makundi ya watu wenye msimamo mkali nchini Indonesaia kwa kutaka kuandaliwa huko.

JESHI LA POLISI LAPIGA MARUFUKU MAANDAMANO YA F, CHADEMA NA NCCR HAPO JUMAMOSI


Jeshi la Polisi Jijini Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano ya umoja wa vyama vya CUF, NCCR na CHADEMA siku ya Jumamosi yaliyokuwa yamepangwa  kuanzia Tazara hadi Jangwani na Mwenge hadi Jangwani na sehemu mbalimbali ...

Taarifa  iliyotolewa  na kamanda Kova  kupitia  ITV   imeeleza  kuwa  Polisi wamechunguza na kugundua kwamba  maandamano  hayo  yataleta usumbufu kwa watu wengine na kwamba kwa kuwa lengo ni kufika Jangwani basi Viongozi wa vyama hivyo wawaambie wafuasi wao waende Jangwani bila Maandamano.

Source: ITV HABARI SAA 2 usiku

MILIONI 58 ZAPATIKANA mechi SIMBA SC, MGAMBO TANGA

Boniface-Wambura1 655d3
MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Simba SC na Mgambo Shooting Stars iliyochezwa jana (Septemba 18 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam umeingiza Sh. 58,365,000.

Watazamaji 10,241 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 23 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa wenyeji Simba kuibuka na ushindi wa mabao 6-0.

Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 13,839,327.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 8,903,135.59.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,036,946.16, tiketi sh. 2,548,890, gharama za mechi sh. 4,222,167.70, Kamati ya Ligi sh.
4,222,167.70, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,111,083.85 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,641,954.10.

Wakati huo huo; Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa siku 14 kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na za Ligi ya Daraja la Kwanza (FDL) kuwasilisha mikataba ya makocha wao.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana Septemba 12 mwaka huu imebaini klabu nyingi hazijawasilisha mikataba ya mabenchi yao ya ufundi, kitu ambacho ni matakwa ya kikanuni. Siku hizo 14 zimetolewa kuanzia Septemba 17 mwaka huu.

Kwa klabu ambazo zitashindwa kuwasilisha mikataba hiyo na vielelezo vingine ndani ya mudau huo zitachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni. Chanzo: TFF

SITTA AWATETEA WAHAMAJI HARAMU...!!!


Ataka operesheni ifanywe kibinaadamu

• Ahoji kama Watanzania nao watafukuzwa itakuaje

Na Fatuma Kitima,DSM

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, ametoa wito kwa mamlaka zinazohusika katika operesheni ya kuwasaka wahamiaji haramu kutumia ubinadamu zaidi katika utelezaji wa zoezi hilo.

Hayo yalisemwa jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Sitta alikiri kuna mapungufu katika zoezi hilo na kusema amri ya rais inatakiwa kutekelezwa lakini kwa kuzingatia haki za binaadamu.

ICC YATAKA MAREKANI IMKAMATE RAIS BASHIR

al-bashir_bcdb9.jpg
Siku mbili baada ya Rais wa Sudan kuiomba Marekani kumpa Visa ya kusafiri nchini humo kuhudhuria mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, wito umetolewa kwa taifa hilo kumkamata Bashir na kumkamabidhi kwa mahakama ya ICC.
Mkutano huo utafanyika wiki ijayo.
Ombi hilo limetolewa na ICC kwa Marekani na kuitaka impe Visa Bashir na kisha kumkamata na kumkabidhi kwa mahakama hiyo pindi tu atakapotua nchini humo.
Bashir anatakikana na mahakama ya ICC kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu na pia kuamuru mauaji ya halaiki katika jimbo la Darfur.
Marekani ilisema kuwa ilipokea ombi la Bashir kutaka Visa na kulitaja ombi hilo kama la kuudhi na kejeli kubwa kwa taifa hilo. Ilimtaka Bashir kwanza kujikabidhi kwa mahakamya ICC kabla ya kutaka kuingia Marekani.
Hata hivyo Marekani sio mwanachama wa mahakama ya ICC na kwa hivyo , kisheria sio lazima itimize matakwa ya mahakama hiyo juu ya Bashir.
Marekani imekuwa katika msitari wa mbele kutaka Bashir akamatwe kwa madai ya uhalifu dhidi yake ili akabiliwa na sheria za kimataifa
Shirika la habari la Reuters lilisema kua mahakama imeshauri Marekani kumkamata Bashir na kumkabidhi kwa ICC ikiwa ataingia nchini humo.
Vibali viwili vya kumkamata Bashir vilitolewa mwaka 2009 na 2010 kwa madai ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Hata hivyo Sudan imepuuza hatua ya ICC kumtaka Bashir kwa makosa ya Darfur wakisema kuwa madai hayo yameongezwa chumvi, na nchi hiyo imekataa kuitambua mahakama hiyo ikisema kuwa ni sehemu ya njama ya nchi za magharibi dhidi ya Afrika.

RAIS KIKWETE AWASHUKIA WANASIASA

 
Rais Jakaya Kikwete
 
*Asema hatawatetea wauza ‘unga’
*Ashangazwa na kiwango cha uongo

RAIS Jakaya Kikwete, amesema anashangazwa na kiwango cha uongo cha baadhi ya wanasiasa ambao hakuwataja majina, kuwa wamekuwa wakizusha madai kuwa Rais aliteua wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, bila kuongozwa na mapendekezo ya wadau mbalimbali waliopendekeza majina hayo.
Alisema bado anaendelea kuamini mchakato wa Katiba mpya utafikia mwisho wake mwaka 2014 na hivyo kuiwezesha Tanzania kufanya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, chini ya Katiba mpya.

Alisema hana tatizo na watu wanaopinga sera za serikali ama hata kumpinga yeye binafsi, bali tatizo lake ni wanasiasa na wanaharakati wanaochochea ghasia, fujo na uvunjifu wa amani.

Rais Kikwete, aliyasema hayo juzi, mjini San Rafael, California, nchini Marekani, wakati alipokutana na kuzungumza na jumuia ya Watanzania waishio katika Jimbo la California.

Katika hotuba yake, ambayo alizungumzia mambo mbalimbali, Rais Kikwete aligusia mjadala wa karibuni bungeni kuhusu mchakato wa Katiba mpya na kusema kuwa alishangazwa na madai kuwa yeye kama Rais, hakuongozwa na mapendekezo ya wadau wakati anateua Tume ya Katiba.

NAPE AWACHONGANISHA CHADEMA NA WAKULIMA WA PAMBA


blog_756b7.jpg
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa wilaya ya Bariadi kwenye Viwanja vya Sabasaba. Adai wamechukizwa na viwanda vya nguo,nyuzi ,nyama na ajira. -Asema misaada ya China ni ukombozi mkubwa unaowakera Chadema. -Awataka kanda ya ziwa kuujua unafiki huo wa Chadema.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya Chadema kukerwa na hatua za Balozi wa China na serikali ya China kwa ujumla katika kushiriki katika hatua za kuwakwamua watanzania katika umasikini.

Nape alisema hayo jana alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mji wa Bariadi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya CCM sabasaba Mkoani Simiyu.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...