Thursday, September 5, 2013

MWANAMKE AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA UWANJA WA NDEGE JNIA LEO MCHANA JIJINI DAR ES SALAAM TANZANIA

Jitihada za kurejesha heshima kwa viwanja vya ndege nchini zilizoanzishwa na waziri wa uchukuzu Dk. Harisson Mwakyembe zinaonekana kuzaa matunda baada ya mwanadada kutoka nchini Nigeria Anthonia Ojo (25) kukamatwa na kete 99 za madawa ya kulevya Dar es Salaam leo.

Zifuatazo ni picha mbalimbali za tukio zima la kunaswa kwa mtuhumiwa huyo ambapo anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi wakati kete hizo zimepelekwa kwa ofisi ya Mkemia Mkuu kwa uchunguzi zaidi. 

ANTHONIA OJO AKIWASILI KITUO CHA POLISI CHA JNIA BAADA KUKAMATWA.
ANTHONIA OJO AKIELEKEA KWENYE GARI BAADA YA KUKAMATWA

WAZAZI WATELEKEZA WATOTO HOTELINI KWA MIEZI MITATU, WADAIWA MILIONI 3

Na Steven Kanyeph - SHINYANGA 
Wazazi ambao hawajulikani makazi yao maalumu wameitelekeza familia ya watoto wao wanne katika hoteli ya Ibanza iliyopo mjini Shinyanga kwa takribani miezi 3 ambapo mpaka sasa wanadaiwa kiasi cha shilingi milioni tatu. 

Mhasibu wa Hoteli hiyo bwana Julius Kiungu amemtaja bi Christina Peter ambaye ni mzazi wa watoto hao kuwa alifika katika hoteli ya Ibanza Mei, 15 mwaka huu akiwa na watoto wa wanne kwa lengo la kupumzika. Bi Chritina ambaye ni mzazi wa watoto hao alieendelea kuwepo katika hoteli hiyo kwa takribani wiki mbili lakini baada ya hapo aliondoka bila taarifa na kuwatelekeza watoto wake katika hoteli hiyo. 

Mmoja wa watoto hao aliyejitambulisha kwa jina la Teddy Masumbuko mwenye umri wa miaka 20 amesema kuwa anashangazwa na kitendo cha mama yao kuondoka bila kutoa taarifa huku akimuacha na wadogo zake watatu wenye umri mdogo. Msemaji wa hoteli hiyo bwana Julius Kiungu anawaomba ndugu, jamaa na marafiki wa familia hiyo wafike ili kuwachukuwa watoto hao kwa ulinzi na usalama wa watoto hao.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...