Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Waziri Mkuu mstaafu Joseph Warioba akisaidiwa kutolewa katika vurugu
Katika
mazingira ya kutatanisha, jana Jumapili Novemba 02, mwaka huu vurugu zimekatisha mdahalo
uliokuwa ukiendelea kujadili mchakato wa katiba mpya ya Tanzania huku
baadhi ya watu wakipigwa na kujeruhiwa.
Mdahalo huo uliokuwa
ukitangazwa moja kwa moja kupitia redio na televisheni za hapa nchini ulivurugika
kutokana na kundi la vijana wapatao 20 kuanza kumzomea aliyekuwa
mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba,
alipokuwa akiwasilisha mada yake. Vijana hao ambao haijajulikana
walitokea wapi au walikuwa na ajenda gani waliinua mabango ya kupinga
msimamo wa waliokuwa wakiendesha mdahalo na kusema rasimu ya katiba
iliyopendekezwa inakidhi mahitaji yote na kusema hakuna haja ya mdahalo. Jaji
Warioba ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania alifanikiwa kutoka
salama nje ya ukumbi ulipokuwa ukifanyika mdahalo huo jijini Dar Es Salaam,
lakini wapo watu waliojeruhiwa kutokana na kurushwa viti na vitu
vingine. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Jeshi
la Burkina Faso limefyatua risasi hewani kuwatawanya waandamanaji nje
ya kituo cha utangazaji cha taifa katika mji mkuu, Ouagadougou.
Ripoti zinasema kuwa risasi zilifyatuliwa punde baada ya kiongozi wa upinzani, Sara Sereme, kuwasili pamoja na wafuasi wake. Wanajeshi waliwatawanya maelfu ya waandamanaji waliokusanyika katika medani kuu mjini Ouagadougou. Vyama vya upinzani vinataka iwekwe serikali ya muda ya raia hadi uchaguzi wa rais utapofanywa. Mjumbe
wa Umoja wa Mataifa mjini humo, Mohamed ibn Chambas, ameonya kuwa
Burkina Faso inaweza kuwekewa vikwazo iwapo jeshi litaendelea kuongoza
nchi. Asante kwa kutembelea blog hii, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz