MJAMZITO
wa miezi nane na nusu ni miongoni mwa mateka waliouawa katika uvamizi
wa kituo cha biashara cha Westgate jijini Nairobi Jumamosi, imefahamika.
Elif
Yavuz ambaye ni msomi wa Chuo Kikuu cha Havard, Marekani aliuawa pamoja
na mumewe Ross Langdon (33) ambaye ni msanifu majengo mwenye uraia
pacha wa Uingereza na Australia.
Taarifa
zilizopatikana jana kutoka eneo la tukio zilisema Langdon ameshiriki
miradi mbalimbali barani Afrika, ikiwamo inayohusika na ujenzi upya wa
hospitali ya Ukimwi nchini Kenya bila malipo yoyote.
Elif
ambaye alikuwa akitarajiwa kujifungua wiki mbili zijazo, aliuawa
sambamba na mumewe huyo ambaye alipata kuwa mshindi wa tuzo ya ujenzi.
Langdon
alipata mafunzo ya ujenzi katika Chuo Kikuu cha Tasmania kisha Chuo
Kikuu cha Sydney, na kufanya kazi katika kampuni kadhaa kabla ya
kuanzisha Kampuni yake ya Regional Associates Ltd, Mei 2008.
Akizaliwa na kukulia Kusini Mashariki mwa Tasmania, miongoni mwa miradi aliyoshiriki iko Uganda, Rwanda na Tanzania.
Alikuwa
mtaalamu wa masuala ya malaria akifanya kazi Kenya katika Wakfu wa
Bill, Hillary and Chelsea, ulioanzishwa na Rais wa zamani wa Marekani,
Bill Clinton, Yafuz pia alipata kufanya kazi na Wakfu wa Bill and
Melinda Gates unaoendeshwa na bilionea muasisi wa Microsoft, Bill Gates.
Akizaliwa
Uholanzi, Yavuz ameishi Cambridge, Massachusetts, wakati akisoma Chuo
Kikuu maarufu duniani cha Havard. Esther Waters-Crane, mtaalamu wa
Uingereza ambaye anamfahamu vizuri Elif, alielezea masikitiko yake kwa
kumpoteza mama huyo mtarajiwa na jinsi Kenya ilivyoshughulikia
shambulizi hilo lisilo na sababu.