Tuesday, March 20, 2018

TRUMP APENDEKEZA ADHABU YA KIFO KWA WAUZA MADAWA YA KULEVYA

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa anataka kuweka adhabu kali ikiwemo adhabu ya kifo kwa wale watakaobaninika kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya. Hatua amesema ni kwa lengo la kukabiliana na ongezeko kubwa watumiaji ndani ya Marekani.
Katika hotuba yake aliyoitoa akiwa New Hampshire,wauzaji wa dawa za kulevya wamesababisha vifo vya maelfu ya watu, lakini cha ajabu baada ya kuhukumiwa kufungwa wanakaa muda mfupi tu gerezani jambo ambalo anasema haliridhishwi nalo.
Ameongeza kuwa tatizo hili linaweza kuondolewa kwa kutumia akili na kuwa imara pamoja na kutenga fedha.
"Mwezi oktoba tulitangaza tatizo hili kama janga la dharula kiafya ambalo limedumu kwa muda mrefu tangu kipindi kilichopita.Tumelifanyia kazi na bunge kuhakikisha tunatenga kiasi cha dola billion sita katika bajeti mpya yam waka 2018/2019 ili kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya,ambapo tutakuwa tumetenga kiasi kikubwa cha fedha kuwahi kutokea dhidi ya tatizo hili'.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MARCH 20, 2018 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


Tunapenda kuwataarifu wadau wa Jambo Tz kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...