Sunday, September 14, 2014

PINDA "KUTAJWA URAIS NI VYEMA"


Waziri Mkuu Mizengo Pinda. PICHA|MAKTABA 


Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema kuwa siyo jambo baya kwake kutajwa kutaka kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao 2015 na kwamba kujitokeza pia ni jambo jema.

 Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake mjini Dodoma juzi, ambapo alizungumzia mambo mbalimbali, Pinda alisema kuwa jambo la msingi kwa wote wenye nia ya kuwania nafasi hiyo ya juu ya uongozi nchini ni kutambua kuwa urais ni dhamana kutoka kwa wananchi na haupatikani kwa uamuzi wa anayegombea, bali taratibu za vyama na wananchi watakaopiga kura.

 Pinda maarufu kama Mtoto wa Mkulima alisema pia kwamba ni muhimu kwa watu wanaotaka kuwania urais wasikiuke misingi ya haki kwa kuingilia mchakato na kuwadhoofisha watu wenye mamlaka ya kuchagua mgombea urais, bali waachwe ili wafanye uamuzi wa haki kwa manufaa ya taifa, huku akisisitiza kufuatwa kwa taratibu za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Kujitokeza ni jambo jema, kutajwatajwa nako pia ni jambo jema tu kwa maoni yangu. Ninachoweza kusema kikubwa, wote wanaotaka kwenda kwenye hiyo nafasi, rai yangu kubwa ni moja tu, watambue wanachotaka kwenda kufanya ni dhamana. Ni nafasi kubwa, lakini ni dhamana tu unapewa kwa niaba ya Watanzania wengine wote.Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAAFISA 10 WAKATAA KURUDI NCHINI LIBERIA

Rais Sirleaf Johnson wa Liberia
Rais wa Liberia Sirleaf Johnson amewafuta kazi maafisa kumi wa serikali kwa kukataa kurudi nchini humo wakati ambapo taifa hilo linakabiliana na maambukizi hatari ya ugonjwa wa Ebola.
Maafisa hao waliagizwa kurudi nchini humo mwezi mmoja uliopita.
Rais Sirleaf amewashtumu kwa kutojali janga linalowakumba raia wa taifa hilo.
Bi Sirleaf ameripotiwa kuomba msaada zaidi kwa serikali ya rais Obama ili kukabiliana na virusi hivyo.
Ameitaka Marekani kujenga kituo kimoja cha kuwatibu wagonjwa wa Ebola katika mji mkuu wa Monrovia.
Virusi hivyo vimewaua zaidi ya watu 2,400 Magharibi mwa Afrika tangu mwezi Machi ,nusu ya raia hao wakitoka nchini Liberia. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MATEKA MWINGINE AKATWANKICHWA NA IS

David Haines
Serikali ya Uingereza imesema kuwa inachukua hatua za dharura ili kubaini ukweli wa kanda ya video inayoonyesha mateka wa Uingereza David Haines aliyetekwa nyara na kundi la himaya ya kiislamu akikatwa kichwa.
Mfanyikazi huyo wa misaada aliyekamatwa nchini Syria mnamo mwezi Machi mwaka jana ameonyeshwa akipiga magoti katika jangwa, kando yake akiwa ni mtu aliyeficha uso wake ambaye amebeba kisu.
Atakuwa mateka wa tatu wa magharibi kukatwa kichwa katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.
katika kanda hiyo ya Video mtu aliyeshika kisu anaonekana akishtumu mataifa yanayounga mkono Marekani,naye Haines ambaye anaonekana kuwa chini ya shinikizo anaonekana akimlaumu waziri mkuu nchini Uingereza David Cameron kwa hatma yake.
Mwisho wa kanda hiyo mateka wa pili wa Uingereza anaonyeshwa na kutishiwa.
David Cameron
Wakati huohuo Waziri mkuu nchini Uingereza David Cameron ameshtumu kukatwa kichwa kwa David Haines kama kitendo cha kishetani.
Amesema kuwa wauaji watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria ata iwapo itachukua mda mrefu.
Katika taarifa yake rais Obama pia ameshtumu mauaji ya kikatili ya David Haines.
Amesema Marekani inaomboleza na Uingereza kifo cha mateka huyo na kungezea kuwa itashirikiana na muungano mkubwa wa kimataifa ili kuwakamata washukiwa mbali na kuharibu tishio hilo kwa ulimwengu.
Wanahabari wawili Steven Sotlof na james Foley waliuawa na wapiganaji hao mwezi uliopita. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...