Tuesday, May 19, 2015

EU KUPAMBANA NA WAHAMIAJI HARAMU

Wahamiaji wakiwa wameketi katika kituo kimoja mjini Tripoli wakiwa na matumaini ya kufika Ulaya

Umoja wa ulaya umekubali kuanzisha kikosi cha Jeshi la wanamaji kwa ajili ya kupambana na wafanya biashara wanaosafirisha watu kutoka Libya.

Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa EU, Federica Mogherini, amesema nia ni kuvunja mtandao unaowasafirisha wahamiaji kupitia bahari ya Mediterania.

NKURUNZIZA AWAFUKUZA KAZI MAWAZIRI WATATU


Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, amewafuta kazi mawaziri watatu, huku maandamano yakiendelea katika mji mkuu kufuatia jaribio la mapinduzi, juma lililopita. 

Mawaziri walioachishwa kazi ni wa Ulinzi, mashauri ya nchi za kigeni na biashara. 

Mapema hii leo, polisi walifyatua risasi hewani katika mji mkuu Bujumbura, kujaribu kuutawanya umati wa vijana uliokuwa ukifanya ghasia.

WEST BROM YAIFUNGA CHELSEA 3-0

Saido Berahino akishangilia goli 

West Brom imewachabanga mabingwa ligi kuu ya England Chelsea jumla ya mabao 3-0 hali ambayo kwa sasa inaifanya klabu hiyo kukaa eneo salama zaidi dhidi ya kushuka daraja. 

Katika mechi hiyo iliyochezwa, dimba la The Hawthons, Saido Berahino alikata utepe wa magoli kwa kufunga goli la kwanza mnamo dakika ya 9, na pia dakika ya 47 Berahino tena akaweka kimiani goli la pili kwa njia ya penati, baada ya kuangushwa na John Terry eneo la adhabu na hivyo hadi mwisho wa mchezo West Brom 3 Chelsea mabingwa nunge. 

Kwa matokeo hayo West Brom sasa wamefanikiwa kukaa eneo salama kuepuka kushuka daraja, huku Chelsea wakiwa bado mabingwa. Kesho Arsenal watakwaana na Sunderland.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...