Serikali za Rwanda, Uganda, Kenya na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, zimefunguliwa kesi katika Mahakama ya Afrika ya Mashariki, zikidaiwa kukiuka mkataba wa kuanzishwa kwa jumuiya hiyo.
Hatua hiyo inatokana na Serikali hizo kufanya vikao vitatu mfululizo na kuzitenga nchi za Tanzania na Burundi.
Walalamikaji katika kesi hiyo, ni Ally Msangi, David Makata na , John Adam, ambao ni Watanzania, wanaotetewa na wakili Mwandamizi, Jimm Obedi wa jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, walalamikaji wamewaomba majaji katika mahakama hiyo, kutoa tamko la kusitisha utekelezaji wa maazimio yote ya vikao vya wakuu wa nchi hizo tatu.
Pia wameomba majaji watoe tamko la kukomesha kurejewa kwa vikao kama hivyo kinyume cha mkataba wa jumuiya hiyo.
Kesi hiyo ya aina yake, ilifunguliwa
jana katika Mahakama ya Afrika ya Mashariki na kupokewa na Ofisa
Masijala i katika mahakama hiyo, Boniface Ogoti.
Kufunguliwa kwa kesi hiyo, kunakuja
siku kadhaa baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzilalamikia nchi hizo, kuhusu
kuitenga Tanzania kwa kufanya mikutano mbalimbali ya maendeleo ya nchi
zao. Nchi nyingine iliyotengwa ni Burundi.
Kikao cha kwanza cha pamoja
kilifanyika Aprili mjini Arusha kabla viongozi hao kukutana Juni 25 na
26 jijini Entebbe nchini Uganda, walidai kuwa na nia moja ya kurahisha
mawasiliano katika nchi hizo.
Mkutano mwilingine ulifanyika mjini
Kigali Rwanda Oktoba 28 ukiwajumuisha Rais Yoweri Museven wa Uganda,
Uhuru Kenyatta (Kenya), Salva Kiir (Sudan Kusini) na Paul Kagame.
Wakili wa walalamikaji Obedi, alisema
katika kesi ya msingi, wanawashtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya
Rwanda, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Uganda,Mwanasheria Mkuu wa
Serikali ya Kenya na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo.
No comments:
Post a Comment