Jeshi
la polisi mkoani Iringa linamshikilia mwalimu wa shule ya msingi
Makungu wilaya ya Mufindi Bw Edwin Ambukile kwa tuhuma za kuwasaidia
majibu wanafunzi wa darasa la saba katika mtihani wa Taifa wa
kuhitimu elimu ya msingi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Bw Ramadhan Mungi amesema kuwa tukio hilo limetokea Septemba 15 mwaka huu .
Alisema kuwa mwalimu huyo ambae ni
mwalimu wa masomo ya Sayansi katika shule hiyo pia alikuwa ni mwalimu
wa masomo ya ziada ( katika shule hiyo na sababu ya kuwasaidia
wanafunzi majibu ni kutaka kupata umaarufu kwa wanafunzi watano
aliokuwa akiwafundisha masomo ya ziada aliopata kuwaahidi kuwa
watafaulu mtihani huo.
Alisema kuwa mwalimu huyo tarehe 11
septemba alipokea mitihani kutoka kwa msimamizi na baada ya hapo
akafungua bahasha ya masomo ya Sayansi na kuanza kufanya mwenyewe
na majibu kuyatuma kwa Sms kwa mke wake .
Hata hivyo siku ya mtihani mmoja kati
ya wanafunzi waliopata majibu hayo alipoingia katika chumba cha
mtihani alionekana akitetemeka kupita kiasi na hivyo msimamizi wa
mitihani alipompekua alimkuta na majibu hayo na kueleza jinsi
alivyosaidiwa na mwalimu huyo .
Kamanda wa polisi alisema siku ya
mtihani mwalimu Ambukile alipangiwa kusimamia shule ya msingi Igomaa
na sasa amekamatwa na atafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia
sasa.
No comments:
Post a Comment