Thursday, October 2, 2014

RAILA ODINGA ATANDIKWA BAKORA HADHARANI...!!!

Mzee Mdzombo anasemekana kutokuwa timamu kiakili
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amemsamehe mzee aliyempiga bakora katika mkutano wa hadhara wa kisiasa katika jimbo la Kwale Pwani ya Kenya,
Mwanamume huyo, Lengo Mdzombo, anayefanya kibarua katika shamba moja Kwale, alikamatwa Jumanne na kufikishwa mahakamani.
Alishitakiwa kwa kosa la kumshambulia kiongozi huyo pamoja na gavana wa Kwale.
Hali ya taharuki ilitanda katika mkutano wa hadhara Jumatatu wiki hii baada ya Mdzombo kwenda ukumbini na kuanza kumtandika bakora kiongozi wa upinzani Raila Odinga pamoja na wanasiasa wengine.
Raila alikuwa amejiunga na kikundi cha wanawake waliokuwa wanacheza densi ya kitamaduni kuwatumbuiza wageni, pamoja na gavana wa jimbo la Kwale Pwani ya Kenya Salim Mvuruya katika mkutanmo wa kisiasa.
Raila alikuwa ameambatana na viongozi wengine, wakiwemo, Seneta Juma Boy, Hassan Omar, Agnes Zani, James Orengo, Johnstone Muthama na wengineo.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga
Mzee huyo alimpiga bakora Odinga ambaye ni waziri mkuu wa zamani kabla ya kumgeukia gavana wa jimbo hilo na kumchapa mara mbili. Hata hivyo mwanamume huyo alishindwa nguvu na walinzi wa Raila Odinga.
Polisi walithibitisha kuwa walimkamata mwanamume huyo na kumwachilia baada ya kugundua kuwa alikuwa na matatizo ya kiakili.
Haijulikani kwa nini mwanamume huyo alimshambulia Raila ila baadhi wanasema ni kwa sababu alighadhabishwa pale waziri mkuu alipocheza densi na mwanamke aliyesemekana kuwa mke wake ambaye alikuwa katika kikundi cha wanawake waliokuwa wanawatumbuiza wageni waheshimiwa.
Viongozi waliofika walilazimika kusitisha densi hiyo kabla ya mwanamume huyo kushindwa nguvu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

MKUU WA USALAMA MAREKANI JIUZULU

Julia Pierson mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Marekani
Mkuu wa Idara ya Usalama nchini Marekani, aliyekuwa na jukumu la kumlinda Rais Barack Obama, amejiuzulu kufuatia matukio yenye kuhatarisha usalama wa taifa yaliyotokea.
Mkuu huyo wa usalama Julia Pierson alikabidhi barua ya kujiuzulu kwa Waziri wa Usalama wa Ndani, Jumatano.
Siku moja kabla, alikabiliana na maswali ya wajumbe wenye hasira kutoka Baraza la Congress juu ya udhaifu mkubwa wa usalama wa Ikulu ya Marekani
Habari za tukio lingine likimhusisha mtu mwenye silaha kuruhusiwa kuingia katika lifti moja na Bwana Obama kulizidisha kutolewa wito wa kumtaka mkuu wa usalama kujiuzulu.
"Leo, Julia Pierson, mkurugenzi wa usalama wa taifa wa Marekani, amenikabidhi barua ya kujiuzulu, na nimeikubali," Waziri wa Usalama wa Taifa Jeh Johnson aliandika katika taarifa.
"Nampongeza kwa utumishi wake wa miaka 30 katika idara ya usalama na taifa." Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

ARSENAL YAUA 4-1, WELBECK APIGA HAT-TRICK


Mshambuliaji Danny Welbeck akishangilia baada ya kupiga 'hat-trick'.

Alexis Sanchez akiifungia Arsenal bao la tatu dhidi ya Galatasaray.

Welbeck akitupia bao la nne. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ametimiza miaka 18 akiwa meneja wa klabu hiyo leo.
KLABU ya Arsenal imetoa kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Galatasaray kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopigwa Uwanja wa Emirates jijini London usiku huu.
Mshambuliaji Danny Welbeck ametupia kambani mabao matatu 'hat-trick' huku bao la nne likiwekwa kimianai na Alexis Sanchez. Katika mtanange huo, kipa wa Arsenal, Wojciech Szczesny alizawadiwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi mshambuliaji wa Galatasaray, Burak Yilmaz.
Ushindi wa leo wa Arsenal umeongeza furaha kwa Meneja wa timu hiyo, Arsene Wenger aliyetimiza miaka 18 akiwa kocha wa klabu hiyo leo.
VIKOSI: 
Arsenal: Szczesny, Chambers, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Flamini, Cazorla, Ozil (Wilshere 77), Sanchez (Ospina 62), Oxlade-Chamberlain (Rosicky 68), Welbeck.
Waliokuwa benchi: Coquelin, Bellerin, Campbell, Podolski.
Galatasaray: Muslera, Chedjou, Felipe Melo, Semih Kaya, Veysel (Bulut 68), Yekta (Altintop 46), Dzemaili, Telles, Sneijder, Pandev (Bruma 68), Burak Yılmaz.
Waliokuwa benchi: Bolat, Balta, Adin, Camdal. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...