Sunday, November 17, 2013

TAIFA STARS SASA KUIKABILI ZIMBABWE J4


Taifa Stars sasa inacheza na Zimbabwe mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date itakayofanyika keshokutwa Jumanne (Novemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Awali Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilikuwa icheze na Kenya (Harambee Stars), lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF) lilituma taarifa jana jioni (Novemba 16 mwaka huu) likieleza kuwa timu yake haitacheza tena mechi hiyo.

Kikosi cha Zimbabwe chenye msafara wa watu 30 kinatarajia kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kesho (saa 3 asubuhi) tayari kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 11 kamili jioni.

NIGERIA YA KWANZA KUKATA TIKETI YA BRAZIL 2014 BAADA YA KUIFUMUA ETHIOPIA 2-0

article-2508386-1973888200000578-737_634x423_5ac75.jpg
Timu ya taifa ya Nigeria imekua nchi ya kwanza ya Afrika kukata tiketi ya kecheza. Fainali za Kombe la Dunia mwakani baada ya ushindi wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Ethiopia leo. Victor Moses alifunga kwa penalti dakika ya 20 na Victor Obinna akaongeza la pili dakika ya 82 kwa mpira wa adhabu, hivyo Super Eagles kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 4-1, baada ya awali kushinda 2- mjini Addis Ababa mwezi uliopita katika mchezo wa kwanza

IVORY COAST NAYO YAFUZU KOMBE LA DUNIA BAADA YA SARE YA1-1 NA SENEGAL

IvoryCoast-celebrates130122G300_2ccf2.jpg
TIMU ya taifa ya Ivory Coast imefuzu Fainali zijazo za Kombe la Dunia baada ya sare ya 1-1 usiku huu ugenini na Senegal kwenye Uwanja wa Mohamed V in Casablanca, Morocco.
Matokeo hayo yanaifanya Didier Drogba na wenzake wafuzu kwa ushindi wa jumla wa 4-2 na kuungana na Nigeria iliyoitoa kwa jumla ya mabao 4-1 Ethiopia.
Ikiwa inajivunia ushindi wa 3-1 katika mchezo wa kwanza, Tembo walilazimika kusota kusawazisha bao baada ya Moussa Sow kutangulia kuwafungia Simba wa Teranga kwa penalti, kabla ya Salomon Kalou kusawazisha dakika za majeruhi.
Kikosi cha Senegal: Coundoul, S. Sane, L. Sane, Mane, Badji/Saivet dk82, P. Cisse, Mbodji, Gueye, Souare, Djilobodji na Ndoye/Sow 66.
Ivory Coast: Barry, K. Toure, Bamba, Gosso, Zokora, Romaric, Aurier, Y. Toure, Kalou, Gervinho/Sio dk80 na Drogba

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...