Tuesday, November 19, 2013

KAGAME, MUSEVENI NA KENYATTA WASHTAKIWA KORTI YA JUMUIYA

kagamepx_deab7.jpg
Serikali za Rwanda, Uganda, Kenya na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, zimefunguliwa kesi katika Mahakama ya Afrika ya Mashariki, zikidaiwa kukiuka mkataba wa kuanzishwa kwa jumuiya hiyo.
Hatua hiyo inatokana na Serikali hizo kufanya vikao vitatu mfululizo na kuzitenga nchi za Tanzania na Burundi.
Walalamikaji katika kesi hiyo, ni Ally Msangi, David Makata na , John Adam, ambao ni Watanzania, wanaotetewa na wakili Mwandamizi, Jimm Obedi wa jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, walalamikaji wamewaomba majaji katika mahakama hiyo, kutoa tamko la kusitisha utekelezaji wa maazimio yote ya vikao vya wakuu wa nchi hizo tatu.
Pia wameomba majaji watoe tamko la kukomesha kurejewa kwa vikao kama hivyo kinyume cha mkataba wa jumuiya hiyo.
Kesi hiyo ya aina yake, ilifunguliwa jana katika Mahakama ya Afrika ya Mashariki na kupokewa na Ofisa Masijala i katika mahakama hiyo, Boniface Ogoti.
Kufunguliwa kwa kesi hiyo, kunakuja siku kadhaa baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzilalamikia nchi hizo, kuhusu kuitenga Tanzania kwa kufanya mikutano mbalimbali ya maendeleo ya nchi zao. Nchi nyingine iliyotengwa ni Burundi.
Kikao cha kwanza cha pamoja kilifanyika Aprili mjini Arusha kabla viongozi hao kukutana Juni 25 na 26 jijini Entebbe nchini Uganda, walidai kuwa na nia moja ya kurahisha mawasiliano katika nchi hizo.
Mkutano mwilingine ulifanyika mjini Kigali Rwanda Oktoba 28 ukiwajumuisha Rais Yoweri Museven wa Uganda, Uhuru Kenyatta (Kenya), Salva Kiir (Sudan Kusini) na Paul Kagame.
Wakili wa walalamikaji Obedi, alisema katika kesi ya msingi, wanawashtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Rwanda, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Uganda,Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Kenya na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo.

DK MVUNGI AZIKWA KIJIJINI KWAO


1461852_10151999781884339_1203660951_n_f818f.jpg
Aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi alizikwa jana kijijini kwake, Chanjale, Kisangara Juu katika mazishi ambayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wajumbe wa tume hiyo, vyama vya siasa na wananchi.
Akizungumza katika mazishi hayo, Askofu Rogath Kimario wa Kanisa Katoliki Dayosisi ya Same alisema tukio la kushambuliwa lililosababisha kifo chake halikuwa la ujambazi.
Akizungumza wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika Kanisa la Moyo Mtakatifu Yesu la Parokia ya Kisangara Juu iliyopo Chanjale, ambayo pia ilihudhuriwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Arusha, Josephat Lebulu; Askofu wa Jimbo la Mbulu, Beatus Kinyaiya na Askofu Damiani Ngalu wa Geita wote wa Kanisa Katoliki, Askofu Kimario alisema waliofanya mauaji hayo ni wauaji wa kimtandao na kuitaka Serikali kutoa majibu sahihi kuhusiana na tukio hilo badala ya majibu mepesi yasiyofanyiwa utafiti.
Kauli hiyo ilionekana kujibu ile ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova kuwa mauaji ya Dk Mvungi ni tukio la ujambazi.

ERNIE BRANDTS KUREJEA NCHINI JUMAPILI

Ernest_5e767.jpg
KOCHA Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts anatarajiwa kutua nchini Jumapili Novemba 24 kusaini mkataba mpya wa kuitumikia timu hiyo katika mzunguko wa pili.
Brandts amemaliza mkataba wa kuitumikia timu hiyo katika mzunguko wa kwanza ambapo kwa sasa wapo kwenye mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo kwa ajili ya kuingia mkataba mpya.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah Bin Kleb alisema, wameshamalizana na kocha hivyo wanasubili akitua tu nchini Novemba 24 ndio wamsainishe mkataba mpya.

"Brandts anatarajia kutua nchini Novema 24 ambapo ndipo likizo yake itakuwa imefikia tamati kwa ajili ya kuja kukiandaa kikosi kwa ajili ya mzunguko wa pili.
"Mara tu atakapotua ndio tunaingianae mkataba mpya, hadi sasa hatujajua tutamsainisha wa muda gani lakini usiozidi chini ya mwaka mmoja," alisema Bin Kleb.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...