Vichekesho

Mume: Kasimu anajisifu eti mtaa huu katembea na wanawake wote kasoro mmoja tu..

MUME karudi alfajiri kushaanza kuwa kweupeeee

MKE: Jamani ndio unarudi saa hizi ulikuwa wapi?
MUME: Dizasta mke wangu, simu yangu iliisha chaji na tulikuwa tunakunywa na rafiki yangu Devi, akapigiwa simu dada yake kafariki, basi tukachanganyikiwa ikalazimika nikeshe huko mpaka asubuhi hii
MKE: Loh jamani poleni. Ngoja nikutengee maji na nikuweke chai harakaharaka maana nitalazimika nami nitoke asubuhi hii hii
MUME: Unaenda wapi?
MKE: Jamani si nakwenda kwenye msiba wa mwenzetu?
MUME: Nilikuwa sijakumalizia story, asubuhi hii wamekwenda mochwari, haleluya Mungu mkubwa, kumbe yule dada alikuwa kazimia tu
^^^^^
Mke: Heeee, unadhani atakuwa nani huyo mme wangu?

Mme: Katakuwa kale ka-Anitha tu, ndo kanajifanya kalokole..

Mke: Umejuaje mme wangu, yaani kale ndo kagumu na ulokole wake...

* Ielezee ndoa hiyo kwa neno Moja tu........
^^^^^ 
GIRL: Baby, hebu niambie harusi yetu itakuwaje?
BOY: Yaani hii haijawahi kushuhudiwa, ngoja nikupe kionjo kidogo tu
GIRL: Enhee...
BOY: Kwanza siku ya kupeleka mahari nitaswaga zizi zima la ng'ombe napeleka kwa babu yako
GIRL: Ooh baby u care..
BOY: Siyo hivyo tu, baba yako ntamnunulia Range Rover Sport na mama mkwe ntampa Range Rover Evoque
GIRL: Baby u are awesome...
BOY: Halagu mdogo wako wa kiume ntampa Prado Tx, na hapo nimesukutua tu mdomo sijaanza kula....
GIRL: Enhee...na sisi??
BOY: Sisi tutachukua mtaa mzima Oysterbay, kila wiki tutaishi nyumba tofauti
Halafu siku ya harusi yetu tutakodi zile meli zinabeba makontena ndiyo iwe ukumbi wetu, itatupeleka hadi Maldives
GIRL: Baby I love you
BOY: Tukitoka hapo tunaenda honeymoon Bahamas....halafu tunaenda Taiwan shopping ya fenicha, kisha Japan shopping ua electronics, halafu tunaenda Dubai nikununulie vito vya thamani
GIRL: Ooh my sweetheart...halafu tukitoka huko??
BOY: Tukitoka huko nachukua ndoo ya maji nakumwagia uzinduke usingizini na ndoto yako imeishia hapo

 
^^^^^
 
John aliruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospital ya
Vichaa, akapakiwa ktk ambulance hadi karibu na
nyumbani kwake, akaulizwa kwako unapakumbuka?
akajibu ndio nyumba yangu ilee, mara wakatoka
watoto wawili wamevaa uniform akasema watoto
wangu walee wanakwenda shule..
Akatoka mwanamke akasema na mke wangu yulee,
Ghafla akatoka mwanaume john akasema mimi
yuleeeeeeee.... naenda kazini!! JE, NI KWELI
AMEPONA??


^^^^^
Mchaga alinunua mbuzi akamwambia mpishi Nyama nusu ipike pilau na ingine itie kwenye friza. Kichwa fanya supu, miguu fanya mchuzi chukuchuku. Ngozi usitupe tutafanya mswala, utumbo pikia ndizi na mifupa tutawauzia wenye mbwa. Kinyesi kihifadhi kwa mbolea ya bustani.
Mpishi akamuuliza Hutaki na sauti ya mbuzi tufanye ring tone kwenye simu yako? Mchaga akajibu Yesuu! hivi inawezekana? bac fanya hivyo tuwauzie na wengine hiyo ringtone. Chezeya mchaga!


^^^^^
Dogo: mama hivi malaika si wanapaa? 
Mama: ndiyo wanapaa, kwanini umeniuliza hivyo?
Dogo: nimesikia baba jana anamuita dada (housegir) malaika wangu, kwa hiyo nae atapaa?
Mama: ndiyo atapaa kuelekea kijijini kwao kesho, pumbavu zake.


^^^^^
Mchungaji kamfuata pedeshe moja maarufu kwa
kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki;
MCHUNGAJI: Kijana, tuko katika harakati za
kujenga kanisa, jitafutie nafasi katika ufalme wa
mbingu kwa kuchangia ujenzi huu. Na Mungu
atakubariki zaidi
PEDESHE: Samahani Mchungaji haitakuwa vizuri
mimi kuchangia kanisa, fedha zangu ni haramu,
huwa nazipata kwa utapeli na kuuza madawa ya
kulevya.
MCHUNGAJI: Yote ni heri, pesa yako tutatumia
kwa kujenga eneo la choo we toa tu!!!

^^^^^
Jamaa alikuwa anagombana na mkewe,hatimae
akamwambia kwa ukali
"Unajua nimechoka sasa, haya kusanya nguo
zako na........ Kabla hajamalizia sentensi simu
ya mkewe ikaita, kumbe alikuwa ni baba yake.
Basi mzee akaanza kuongea na binti yake huku
jamaa anasikia
"Aisee mwanangu nimebahatika kuuza ile
nyumba yangu sasa nimeona niwatumie milioni
20 mjaribu kuanzisha mradi na mwenzio.
Haya mwambie yeye nitampigia kesho kama
ana mradi mwingine nimpe hela kidogo".Baada
ya simu kukatwa mke akamgeukia jamaa
akamuuliza,"eeenhee!!! ulikuwa unasema
umenichoka nikusanye nguo zangu halafu
iweje? Jamaa kwa upole akajibu "Nilikuwa
nasema ukusanye nguo zako na unipe nifue".

  

^^^^^
WASICHANA WAWILI WAKISAFIRI KATIKA TRENI

Msichana-1: Ni aina gani ya mume ungependa kupata?

Msichana-2: Awe Billionaire

Msichana-1: Nini?! kama hautapata billionaire?

Msichana-2: Basi awe Millionaire

Msichana-1: Je kama hutapata mwenye pesa kiasi hicho?

Msichana 2: Mwenye millioni moja anafaa pia

Msichana-1: Kama sio?

Msichana-2: Mwenye laki tano sio mbaya sana.

(Zuzu akiwa amelala Kitanda cha juu akasikika akinong'oneza)

"Akifika BUKU KUMI(Tsh 10,000) uniamshe!!!!!!"
 ^^^^^
DOKTA alimkuta Chizi Yuko Nje ya Wodi Anachungulia Chini ya Gari!! Dokta akasema; Aah!! Hili Chizi litakua Limepona hadi Linatengeneza Gari!!
ikabidi Amfuate amuulize; Wewe Chizi Unafanya Nini Chini ya Gari??
Chizi akasema; Nilikuwa Nalichunguza Kama
Jike au Dume!!
UNGEKUWA WEWE NDIO DOKTA UNAFANYAJE MWANAWANEEE???

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...