KOCHA Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts
anatarajiwa kutua nchini Jumapili Novemba 24 kusaini mkataba mpya wa
kuitumikia timu hiyo katika mzunguko wa pili.
Brandts amemaliza mkataba wa
kuitumikia timu hiyo katika mzunguko wa kwanza ambapo kwa sasa wapo
kwenye mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo kwa ajili ya kuingia mkataba
mpya.
Akizungumza jijini Dar es Salaam,
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah Bin Kleb alisema,
wameshamalizana na kocha hivyo wanasubili akitua tu nchini Novemba 24
ndio wamsainishe mkataba mpya.
"Brandts anatarajia kutua nchini Novema 24 ambapo ndipo likizo yake itakuwa imefikia tamati kwa ajili ya kuja kukiandaa kikosi kwa ajili ya mzunguko wa pili.
"Mara tu atakapotua ndio tunaingianae mkataba mpya, hadi sasa hatujajua tutamsainisha wa muda gani lakini usiozidi chini ya mwaka mmoja," alisema Bin Kleb.
No comments:
Post a Comment