Tuesday, October 14, 2014

WAZIRI LAZARO NYALANDU AZUNGUMZIA TETESI ZA KUTANUA NA AUNT EZEKIEL NCHINI MAREKANI

  Baada ya vyombo vya habari kuripoti kuhusu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu(Pichani juu) na msanii wa filamu Aunty Ezekiel kuvinjari nchini Marekani hatimaye waziri huyo 
Aunt Ezekiel
alisema tuhuma hizo zimetengenezwa na kundi la watu ambalo miongoni mwao ni baadhi ya viongozi wa Serikali ambao humchafua kutokana na utendaji kazi wake.

Nyalandu alisema alikwenda Marekani septemba12 kwa ajili ya kufungua tamasha la utamaduni na utalii kupitia soko la wasanii wa Tanzania ambako alikutana na msanii huyo mara moja pamoja na mwingine wa Bongo Fleva Kassim Mganga usiku katika moja ya maeneo nchini humo.

Alikana kutanua na msanii huyo kama baadhi ya nyombo vya habari vilivyoripoti na kusema maneno hayo ni kwa lengo la kumwaribia heshima yake mbele ya jamii. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAMA KANUMBA NA LULU NDANI YA FILAMU MPYA IITWAYO "MAPENZI YA MUNGU"

Hivi karibu Msanii Mahiri na Nguli katika tasnia ya filamu nchini Elizabeth Michael almaarufu kama LULU ataibuka na filamu yake Mpya na yenye kusisimua iitwayo "MAPENZI YA MUNGU" ambapo moja kati ya washiriki katika filamu hiyo ni Bi Flora Mtegoha ambae ni Mama Mzazi wa aliyekuwa Msanii Nguli wa Kiume Hapa Bongo Marehemu Steven Kanumba.

Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" ni moja ya filamu ambayo Lulu ameonyesha uwezo wa hali ya na kuthibitisha kuwa ni mmoja kati ya wasanii wa kike hapa Tanzania ambae ana kipaji cha hali ya juu katika kuuvaa uhusika ambapo ana uwezo wa kubadilika badilika kutokana na muongozo anaopewa.

Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" itakuwa Sokoni hivi Karibu Kwa Wauzaji wa Filamu kote Nchini.

Filamu hii itasambazwa na Kampuni mahiri ya Proin Promotions Ltd. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAASKOFU KATOLIKI WAUZUNGUMZIA USHOGA


Mkutano wa maaskofu Vatican

Makasisi wanaoshiriki katika mkutano wa maaskofu wanaangazia masuala ya mafunzo ya kanisa katoliki kwa familia ,wametoa mwito kwa kanisa hilo duniani kuwachukulia watu wenye mapenzi ya jinsia moja kwa usawa
Kauli hii inakuja baada ya Maaskofu kuandika ripoti wakati wa mkutano wa synodi ukiendelea huko Vatican na kusema kuwa wapenzi wa jinsia moja wana zawadi na viwango vya kutoa kwenye jumuiya za kikristo hii ikiwa ni ripoti iliyotolewa mapema wiki hii. Ripoti hiyo haitoi changamoto yoyote kwa msimamo wa muda mrefu wa kanisa hilo juu ya kupinga ndoa za jinsia moja,lakini baadhi ya vikundi vya kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wanachukulia kauli hiyo kuwa ya mafanikio makubwa kwa jamii zao. Na moja ya makundi yenye kushikilia msimamo mkali kikanisa wametupilia mbali ripoti hiyo na kuuita ya kisaliti. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...