Kiongozi huyo ambaye alishangaza watu kwa uamuzi huo wa Februari 8, mwaka huu, hata hivyo alisema sauti ya Mungu imejibu kupitia kwa mfuasi wake, Papa Francis. Papa Benedict alitangaza uamuzi wa kujiuzulu Februari 11, maelezo yake yalielekeza katika afya yake. Alisema nguvu zake zilikuwa zimepungua kiasi cha kutokuweza kumudu majukumu yake ipasavyo. Alisema, "Mungu aliniambia 'niondoke,' nami nikatimiza wajibu huo bila kusita," alisema Papa Benedict ambaye amekuwa kiongozi wa kwanza kufikia uamuzi huo baada ya miaka 600 ya Kanisa Katoliki. Alisema tangu wakati huo ameishi maisha ya sala.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 86 alisema ameshuhudia maono ya Mungu kwa miezi kadhaa huku akisikia sauti na tamaa ya kuendelea kuwa karibu naye (Mungu). Papa Benedict, hata hivyo alisema Mungu amembariki na kumwezesha kuuona utukufu wake kupitia kwa Papa Francis, akielewa kwa nini alitakiwa kuondoka mapema kwa kuitika sauti na utashi wa Mungu. Tembelea http://jambotz8.blogspot.com/ kila siku.