Sunday, April 19, 2015

TAZAMA PICHA ZA MNYAMA ALIVYOCHINJWA NA MBEYA CITY JANA

IMG_9679
WEKUNDU wa Msimbazi Simba wamefungwa magoli 2-0 na Mbeya City katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyochezwa uwanja wa Sokoine Mbeya jioni ya jana.
Kwa matokeo hayo Simba imeendelea kubaki nafasi ya tatu kwa pointi zake 35 baada ya kucheza mechi 22 nyuma ya mabingwa Azam fc wenye pointi 42  baada ya kushinda mechi yao jana mabao 2-1 dhidi ya Kagera. Azam nao wamecheza mechi 22. 
Vinara bado wanabaki kuwa Yanga kwa pointi 46 baada ya kucheza mechi 21.
Magoli ya Mbeya City yalifungwa na Paul Nonga dakika ya 45 kipindi cha kwanza akipokea pasi kutoka kwa Deus Kaseke. City walifunga goli la pili dakika ya 69 kupitia kwa Peter Mwalyanzi.
 Simba ilipata pigo dakika ya 23 baada ya beki wake na nahodha, Hassan Isihaka kuumia na nafasi yake ikachukuliwa na Mganda Joseph Owino
 
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
 Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...