Polisi Zanzibar wameanza
uchunguzi kubaini mazingira ya safari tata ya mtoto Karine Godfrey
aliyesafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar kwa ndege bila tiketi
wala kugundulika.
Mtoto huyo, Karine au Jenipher Godfrey anayesoma
darasa la tatu katika Shule ya Msingi Jitihada, Dar es Salaam alionekana
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Septemba
Mosi saa 11.30 jioni, akieleza kuwa aliingia Zanzibar kwa ndege ambayo
hata hivyo, haikufahamika mara moja ni ya shirika gani.
Alikutwa uwanjani hapo akijiandaa kuondoka kwenda mahali asipopajua.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam
Khamis alisema mbali ya kushangazwa na mazingira ya safari ya mtoto
huyo, polisi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar
wanalifanyia kazi suala hilo.
“Ni jambo la kushangaza. Tunajiuliza, huyu mtoto
alifikaje katika ndege bila ya kuwa na tiketi wala taarifa zozote
kuelezea safari yake na je, huko Dar es Salaam aliondokaje hadi kuingia
katika ndege bila ya hivyo vitu, sielewi ilikuwaje. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“Ina maana hakufanyiwa hata ukaguzi kama ilivyo
kawaida kwa wasafiri. Tunalichunguza hili, huu ni uzembe wa hali ya juu
ulioonyeshwa na wahusika wote wa viwanja vya ndege,” alisema.
Alivyogundulika
Kamanda Khamis alisema kuwa ilikuwa saa 11.30
jioni, mtoto huyo alipogundulika baada ya dereva wa teksi, Kassim Gharib
kumwona akiwa nje ya uwanja huo kwa muda mrefu na kuanza kumhoji.
Katika mahojiano hayo, mtoto huyo alisema alishuka
katika ndege kutoka Dar es Salaam na kwamba anaishi Kitunda pia, Dar es
Salaam. Hata hivyo, alikataa kusema alipanda ndege ya shirika gani.
Alisema lengo la kwenda kwake Zanzibar ni
kumtembelea baba yake mzazi ambaye alimtaja kwa jina moja la Godfrey na
kuongeza kuwa ni askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), lakini
bila ya kueleza yupo kambi gani. Baada ya hapo dereva huyo alimpeleka
Kituo cha Polisi Mazizini.
Ofisa wa Kituo cha Kulelea Watoto chini ya Wizara
ya Uwezeshaji Ustawi wa Jamii, Vijana na Watoto, Khadija Ahmed alisema
mtoto huyo amehifadhiwa katika kituo hicho wakati utaratibu wa kuwapata
ndugu zake ukiendelea.
Alisema baada ya kumhoji zaidi, mtoto huyo alidai
kuwa alisindikizwa uwanjani na dada yake aliyemtaja kwa jina la Angela
na kwamba wanafanya utaratibu wa kuwasiliana na Wizara ya Ustawi wa
Jamii, Jinsia na Watoto ili kufuatilia kwa upande wa Dar es Salaam.
“Alisema anasoma darasa la tatu B, Shule ya Msingi Jitihada na
alimtaja Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo kwa jina la Kihawa na mwalimu wake
wa darasa kwa jina moja la Amos,” alisema Ahmed. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege
Zanzibar, Kapteni Said Ndumbogani alisema wameangalia mikanda ya kamera
ya CCTV na kumwona mtoto huyo akiwa pamoja na abiria wengine katika basi
ambalo huchukua abiria baada ya kuteremka kutoka kwenye ndege.
“Tulitilia shaka kuwa huenda alikuja na ndege ya
(anataja shirika) lakini bado hatuna uhakika ila tulipouliza uongozi wa
shirika hilo ulikataa, hivyo ni vigumu kusema alikuja kwa ndege gani
kwani siku hiyo kulikuwa na ndege nyingi na mtoto hakuonekana akiteremka
kwenye ndege,” alisema Ndumbogani. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment