Sunday, April 19, 2015

MKUU WA KANISA LA ANGLIKANA AZURU MISRI

Justin Welby Katikati
Askofu mkuu wa Cantebury ,Justin Welby anawatembelea viongozi wa kisiasa pamoja na wale wa kidini nchini Misri ili kuzungumzia kuhusu mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya wakristo katika eneo la mashariki ya kati.

Askofu huyo ambaye ndio kiongozi wa Kanisa la Anglikana anatarajiwa kukutana na rais wa Misri Abdul Fattah al Sisi.

Pia atatoa rambirambi zake kwa wakristo wa kanisa la Coptic ambao walitekwanyara na kuuawa na wanamgambo wa Islamic State nchini Libya mnamo mwezi wa Februari.
Askofu huyo amesema kuwa utekajinyara wa wakristo katika eneo hilo ni m'baya zaidi kwa karne kadhaa.

Pia atakutana na Imam mkuu wa chuo cha al-Azhar ambacho ndio taasisi kuu nchini Misri na inaheshimiwa na waislamu wa Sunni kama taasisi kubwa zaidi ya mafunzo ya kiislamu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...