Usiku wa jana watu wawili waliowahi kuwa vipenzi vya nchi ya Ureno –
Jose Mourinho na Nemanja Matic walirejea nchini humo katika jiji la
Lisbon lakini safari hii wakiwa kama wapinzani.
Huku Mourinho akionekana kuchukua ‘attention’ yote ya vyombo vya habari ndani ya jiji Lisbon, Nemanja Matic alikuwa kasahaulika.
Lakini katika dakika ya 34, mchezaji huyo wa zamani wa Benfica aliifungia goli pekee Chelsea katika mchezo huo.
Matic alifunga goli hilo kwa kichwa baada ya kuachwa bila kukabwa vizuri na mabeki wa Sporting Lisbon.
Mchezaji wa zamani wa Manchester United Luis Nani alikuwa akiitumikia
Sporting jana na hakuwa kwenye kiwango kizuri katika kipindi cha kwanza
– kipindi cha pili alijitahidi lakini akashindwa kubadili matokeo ya
mwisho dhidi ya vijana wa Jose Mourinho.
Takwimu na timu zilizopangwa
Sporting (4-3-3): Patricio 7; Cedric 6, Mauricio 5.5 (Oliveira 63, 6),
Sarr 5, J.Silva 5; Mario 6, Carvalho 6, A.Silva 6 (Montero 81); Carrillo
6.5 (Capel 81), Slimani 6, Nani 6.
Subs not used: Marcelo, Jefferson, Martins, Rosell.
Bookings: Carvalho, Mario, Cedric, Mauricio
Manager: Marco Silva
Chelsea (4-2-3-1): Courtois 6; Ivanovic 6, Cahill 6, Terry 6, Luis 6.5;
Matic 8, Fabregas 7; Schurrle 5 (Willian 57, 6), Oscar 7.5 (Mikel 71,
6), Hazard 7 (Salah 84); Costa 6.
Subs not used: Cech, Zouma, Azpilicueta, Remy.
Bookings: Ivanovic, Hazard, Luis Filipe, Fabregas
Manager: Jose Mourinho.