Mwenyekiti wa Taasisi ya Demokrasia Tanzania (TCD), John Cheyo amewavaa viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), akieleza kuwa walichokubaliana katika kikao chao na Rais Jakaya Kikwete ni kwamba Bunge liahirishwe Oktoba 4 na si kama wanavyodai wakiwa nje.
Akizungumza bungeni mjini Dodoma jana, Cheyo
alisema hakuna makubaliano ya kutaka Bunge lisitishwe kabla ya
kukamilisha kazi zake Oktoba 4, ikiwamo kutoa Katiba itakayopendekezwa
kwa wananchi.
“Mojawapo tulilokubaliana ni Bunge hili lipate
Katiba itayopendekezwa kwa wananchi,” alisema Cheyo huku akipigiwa
makofi na kelele kutoka kwa baadhi ya wajumbe.
“Pia tulikubaliana kwa hali halisi ya muda
tulionao, haiwezekani mchakato mzima ukamalizika na maana ya kumalizika
mchakato ni kura ya maoni ya wananchi na ndiyo wenye Katiba.” Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“Tukasema kama inabidi tufike mpaka kule (kura ya
maoni) inatubidi tuahirishe uchaguzi wa 2015 jambo ambalo sisi wote
hatuliafiki na mheshimiwa Rais alisema msinitwishe mzigo huu,”
alisisitiza Cheyo.
Cheyo alisema Rais katika mazungumzo hayo alitaka
utaratibu wa kufanya uchaguzi kila Oktoba ya mwisho wa kipindi cha miaka
mitano uendelee ili wananchi wenyewe watoe ridhaa kupitia uchaguzi wa
viongozi.
“Bunge hili haliendeshwi kwa amri ya mtu ambaye
yuko barabarani. Bunge hili linaendeshwa kwa mujibu wa Sheria na sheria
tuliyokuwa nayo kwa sasa ni GN 254 (tangazo la Serikali) ambayo inasema
uhai wa Bunge ni mpaka Oktoba 4,”alisema Cheyo.
Cheyo alisema haiwezekani Rais akasimama mara
baada ya makubaliano na kutangaza kuwa siku inayofuata Bunge lisitishe
shughuli zake.
“Watu tumekubaliana na kuna video ambayo kila
mmoja aliyekuwa akizungumza alirekodiwa. Kweli mnataka tumuombe sasa
mheshimiwa Rais tutengenezewe kipindi maalumu kila mmoja aonekane
anasema nini?” alihoji.
“Tuwe waungwana. Itoshe mimi kusema yale niliyotangaza hayo ndiyo makubaliano. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment