Baadhi ya wajumbe
wa Bunge la Katiba waliopiga kura za hapana wamelazimika kuondoka Dodoma
na kurudi Zanzibar kwa madai ya vitisho walivyopata kutoka kwa wenzao.
Mmoja wa wajumbe hao, Salma Said alisema jana
jioni kuwa yeye na wajumbe wenzake wamekataa kuitikia wito wa Mwenyekiti
wa Bunge, Samuel Sitta kwenye Kamati ya Mashauriano ili kuhojiwa kuhusu
kura hiyo na kutokana na vitisho wanavyopata kutoka kwa wajumbe wenzao
wameamua kuondoka Dodoma.
Vitisho hivyo vimeripotiwa muda mfupi baada ya
Sitta kuunda Kamati ya Mashauriano ya watu tisa inayoongozwa na Makamu
Mwenyekiti, Samia Suluhu Hassan kushughulikia kura hizo zilizopigwa na
wajumbe saba zinazoweka njiapanda uwezekano wa kupatikana akidi ya
kupitisha Katiba inayopendekezwa.
Wajumbe waliopiga kura za wazi za hapana kwa ibara
zote ni Adil Mohamed Adil, Dk Alley Soud Nassor, Fatma Mohamed Hassan,
Jamila Ameir Saleh, Salma Hamoud Said, Mwanaidi Othman Twahir na Ali
Omary Juma. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Kwa upande wa Tanzania Bara aliyepiga kura ya
hapana kwa rasimu nzima ni Mbunge wa Mpanda Kati (Chadema), Said Arfi na
wajumbe 30 kutoka Zanzibar wakipiga kura ya siri.
“Baada ya kupiga kura za hapana leo (jana),
walijitokeza wajumbe akiwamo (jina tunalihifadhi kwa sasa) wakaanza
kutuzongazonga,” alisema Salma.
“Walituambia kuwa tumebaki hadi dakika ya mwisho
halafu tunasema hapana kwa rasimu nzima ili kula fedha za bure, wanasema
bora tungeondoka na Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi).”
Hata hivyo, alipopigiwa simu yake ya mkononi mmoja
wa watuhimiwa, alipokea na baada ya mwandishi kujitambulisha alikata
simu na alipopigiwa mara ya pili alijibu alisema; “Mimi ni mheshimiwa
mwana na niko Sudan.”
Salma alisema miongoni mwa wajumbe hao wakiwamo
baadhi ya mawaziri waliwafuata hadi nje ya ukumbi wakiwatishia kuwa
watawafanyia hujuma kwa kukataa kuunga mkono rasimu hiyo.
“Sisi tumeamua kuondoka kurudi kwetu, hatutaingia tena bungeni maana hivi vitisho vimezidi sasa,” alisema Salma.
Juhudi za kuwapata wajumbe wenzake kuzungumzia
vitisho hivyo hazikuzaa matunda, lakini Katibu wa Bunge hilo, Yahya
Khamis Hamad alikiri kupokea malalamiko hayo na kwamba amelichukulia
kama suala la kisiasa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Alisema wajumbe hao hawajasema wametishiwa
kufanyiwa kitu gani, bali walimweleza kuwa wameambiwa kuwa wamekaa pale
(bungeni) kwa ajili ya kupata pesa.
Kuhusu kukataa kwao kuhudhuria katika Kamati ya Mashauriano,
Hamad alisema hawezi kulitolea jibu kwa kuwa litafanya maridhiano
yasifanyike.
Kamati ya Maridhiano
Akitangaza kuunda kamati hiyo, Sitta alisema ana
suala mbele yake ambalo linahitaji mashauriano chini ya Kanuni ya 54(4)
kutokana na baadhi ya wajumbe kupiga kura ya hapana kwa ibara zote.
Kanuni hiyo inasema: “Mwenyekiti baada ya
kushauriana na kamati ya uongozi anaweza kuunda kamati ya mashauriano
pale linapojitokeza suala linalohitaji mashauriano.
“Baadhi ya wajumbe jana (juzi), walipiga kura za
hapana kwa ibara zote, jambo ambalo haliwezekani kuwa hivyo. Kwa
kushirikiana na Makamu Mwenyekiti, nimeunda kamati hii ambayo naomba
ikafanye kazi leo,” alisema.
Alisema kamati hiyo yenye wajumbe tisa
itakayoongozwa na Samia na baada ya kikao chake cha jana itatoa matokeo
bungeni. Wajumbe wengine ni Rashid Mtuta, Shamsi Vuai Nahodha, Omary
Yusuf Mzee, Mohamed Aboud, Andrew Chenge, Dk Asha-Rose Migiro, Dk
Francis Michael na Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi.
“Hawa watakaa na wale wawili walioniomba kwamba
wanataka kusikilizwa kwa nini wamesema hapana kwa kitendo ambacho
inaonekana kama wamepoteza muda kukaa bungeni ili kukataa Katiba yote,”
alisema.
Alitoa nafasi kwa wajumbe wengine ambao walipiga
kura za hapana watakaopenda kwenda katika kamati hiyo kueleza ni kwa
nini waliikataa rasimu hiyo.
Hata hivyo, kabla ya kuanza kwa upigaji kura jana,
Sitta alisema kuwa hali inakwenda vizuri... “Inshallah hali inakwenda
vizuri na dua la kuku halimpati mwewe.”
Kwa mujibu wa Kanuni 36(3). Endapo mjumbe baada ya
kukataa ibara za Rasimu ya Katiba, mwenyekiti ataunda kamati ya
mashauriano ambayo itasikiliza hoja zake na kupata mwafaka.
Kanuni 36 (4), baada ya kamati ya mashauriano
kukutana na kujadili ibara inayobishaniwa, itapeleka taarifa ya matokeo
ya mashauriano yake kwenye Bunge Maalumu kwa ajili ya kujadiliwa na
ibara hiyo kama ilivyo au baada ya kuandikwa upya kwa kuzingatia taarifa
ya Kamati ya Mashauriano.
Endapo theluthi mbili haitapatikana kwa mara ya
pili, ibara hiyo itahesabiwa kuwa haikukubaliwa wala kupitishwa na Bunge
Maalumu kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na sheria na kanuni hizi.
TEC yamshukia Sitta
Kauli ya Sitta kuwa baadhi ya nyaraka kuhusu
mchakato wa Katiba Mpya zinazotolewa na makanisani, “hazina utukufu wa
Mungu na ni za kipuuzi” imepondwa na Baraza la Maaskofu wa Kanisa
Katoliki Tanzania (TEC), likisema hajui nguvu ya umma.
Akizungumza na gazeti hili jana, Makamu wa Rais wa
TEC, Askofu Severine Niwemugizi alisema: “Unadhani tulivyotoa waraka
tulikuwa tunawataka waumini wafanye nini? Je, ni kufuata dhehebu lako
limesema nini au kufuata kilichomo katika waraka? Wewe (mwandishi) si
Mkristo? Jibu hilo.”
Aliongeza, “Wenye mapenzi na nchi hii wamfute
kichwani Sitta na huo upuuzi aliosema ni wake mwenyewe. Huyu anadhani
kuwa ana akili kuliko mamilioni ya Watanzania waliopendekeza wanataka
kujitawala namna gani?”
Sitta alitoa kauli hiyo mjini Dodoma juzi wakati
akiwatambulisha viongozi 13 kutoka Jumuiya ya Image ya Kanisa Kuu la
Mtakatifu Paulo wa Msalaba ya mjini Dodoma.
Licha ya Sitta kutotaja taasisi husika, lakini
Jukwaa la Wakristo Tanzania ndilo lililotoa waraka unaotaka kusitishwa
kwa mchakato wa Katiba Mpya na kusambazwa makanisani.
Waraka huo ulitolewa kwa pamoja na TEC, Jumuiya ya
Kikristo Tanzania (CCT), Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania
(FPCT) na Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA).
“Anadhani wanaweza kutunga Katiba ya kuwatawala
wananchi. Kauli aliyoitoa ni sawa na kuwapuuza Watanzania na ni sababu
ya madaraka tu, maana ndiyo yanayowapa watu wengi kiburi,” alisema.
Askofu
huyo alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa
kauli hiyo ya Sitta maana yake ni kwamba CCM itabaki milele madarakani
na Watanzania hawawezi kuwafanya jambo lolote. Kuwa wa kwanza kupata
habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“Unajua mtu mwenye kiburi na dharau anayedhani
hawezi kuambiwa chochote unatakiwa kumwacha kama alivyo ila Watanzania
ndiyo watakaoamua nini wanataka katika maisha yao,” alisema.
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Antony
Lusekelo alisema: “Bunge la Katiba limemwelemea Sitta na ndiyo maana
ameanza kutukana watu.”
Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako alisema kwa
jinsi jamii ilivyogawanyika katika mchakato wa kupata Katiba Mpya,
ilikuwa jambo la busara kwa makanisa kutaka kusitishwa kwa mchakato huo
mpaka makundi yote yanayovutana yafikie mwafaka.
Masheikh waishtukia Serikali
Viongozi wa taasisi mbalimbali za Kiislamu nchini
wamesema hawana imani kuwa Serikali itatekeleza kauli yake kwamba
mwakani itawasilisha bungeni muswada wa sheria ili kutambua Mahakama ya
Kadhi.
Wamesema kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, moja
ya ajenda za CCM ilikuwa ni kuhakikisha kuwa mahakama za Kiislamu
zinatambulika kisheria, lakini licha ya chama hicho kushinda mpaka sasa
ahadi hiyo haijatekelezwa.
Juzi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alilazimika
kuokoa jahazi la ‘kuzama’ kwa Katiba Mpya kwa kupoza hasira za Waislamu
kuhusu mahakama hiyo kutoingizwa kwenye Katiba inayopendekezwa.
Msemaji Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu na
Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Rajabu Katimba alisema: “Waziri Pinda
amesema Januari lakini sisi tunaona wazi kuwa kauli yake haina ukweli.
“Mahakama za Kiislamu zilizopo sasa hazitambuliki
kisheria na tunachokitaka ni kutambulika kwake na maamuzi yake
yasiingiliwe.” Akitolea mfano wa ahadi ya mwaka 2010 alisema, “Mahakama
ya Kadhi ni sehemu ya ibada kwa Waislamu. Ingesaidia kuokoa fedha nyingi
ambazo wanalipwa watumishi wa mahakama kwa ajili ya kusikiliza kesi
zinazoweza kuamuliwa na mahakama za Kiislamu.”
Mwenyekiti wa Taasisi ya Amani ya Kiislamu
Tanzania (TIPF), Sheikh Sadiki Godigodi alisema: “Wasiwasi wangu ni juu
ya utekelezaji wa kauli ya Pinda. Si mara ya kwanza Serikali kusema
jambo hilo lakini halitekelezwi.”
Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Taasisi ya Masheikh
Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, Sheikh Khamis Mataka alisema: “Tulikuwa
na madai ya asilimia 100 lakini Serikali imetupa asilimia 50.
Tunazipokea lakini tunaendelea kudai nyingine 50 kwa sababu si busara
kukataa kupokea nusu ya kitu ulichokiomba.
“Tunaamini Serikali itatekeleza maagizo yake na
kuzifanya mahakama za Kiislamu kutambulika kisheria. Itekeleze jambo
hili kama ilivyoahidi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment