Wenyeji walilazimika kucheza 10 kwa
takriban dakika 80, baada ya beki Adil Rami kutolewa nje kwa kadi
nyekundu, kufuatia kumchezea rafu Wilfried Bony.
Mshambuliaji huyo ndiye aliyeifungia
Swansea bao la kwanza dakika ya 14 usiku huu, hilo likiwa bao lake la
tano katika mechi nanemsimu huu.
Mabao mengine yalifungwa na Michu dakika ya 58 na Jonathan de Guzman dakika ya 62.
Kikosi cha Valencia kilikuwa: Guaita,
Barragan, Rami, Feghouli/Pabon dk59, Mathieu, Ever/Costa dk14, Javi
Fuego, Guardado, Canales/Bernat dk66, Cartabia na Postiga.
Swansea: Vorm, Rangel/Davies dk56,
Amat, Chico, Tiendalli, de Guzman, Canas, Pozuelo, Dyer/Lamah dk65,
Michu/Shelvey dk77 na Bony.
Katika mchezo mwingine, mabao mawili
ya Jermain Defoe yalichgia ushindi wa 3-0 kwa Tottenham dhidi ya Tromso,
bao lingine akifunga Christian Eriksen.
Pamoja na ushindi huo, Mousa Dembele, Danny Rose and Younes Kaboul wote walitoewa nje baada ya kuumia.
Tottenham ilimaliza mechi na wachezaji
10 kutokana na Kaboul kutolewa nje baada ya kuumia, wakati kocha Andre
Villas-Boas amemaliza idadi ya wachezaji wa kubadili.
Spurs: Lloris, Naughton, Kaboul, Dawson, Rose, Sandro, Dembele, Sigurdsson, Holtby, Lamela na Defoe.
Tromso: Sahlman, Kristiansen, Fojut,
Koppinen, Causevic, Bendiksen, Johansen, Drage, Pritchard, Moldskred,
Ondrasek. Chanzo: binzubeiry