Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa anataka kuweka adhabu kali ikiwemo adhabu ya kifo kwa wale watakaobaninika kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya. Hatua amesema ni kwa lengo la kukabiliana na ongezeko kubwa watumiaji ndani ya Marekani.
Katika hotuba yake aliyoitoa akiwa New Hampshire,wauzaji wa dawa za kulevya wamesababisha vifo vya maelfu ya watu, lakini cha ajabu baada ya kuhukumiwa kufungwa wanakaa muda mfupi tu gerezani jambo ambalo anasema haliridhishwi nalo.
Ameongeza kuwa tatizo hili linaweza kuondolewa kwa kutumia akili na kuwa imara pamoja na kutenga fedha.
"Mwezi oktoba tulitangaza tatizo hili kama janga la dharula kiafya ambalo limedumu kwa muda mrefu tangu kipindi kilichopita.Tumelifanyia kazi na bunge kuhakikisha tunatenga kiasi cha dola billion sita katika bajeti mpya yam waka 2018/2019 ili kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya,ambapo tutakuwa tumetenga kiasi kikubwa cha fedha kuwahi kutokea dhidi ya tatizo hili'.
Hata hivyo Rais Trump ameelezea mikakati iliyowekwa tayari katika kukabilianba na dawa za kulevya hadi sasa.
"Kwanza kabisa tunapunguza kiwango uhitaji wa dawa hizo, kuhakikisha tunapunguza idadi ya watu wanaojiingiza na hatimaye kutekewa na matumizi ya dawa za kulevya, ni muhimu sana.
Hiyo inahusisha serikali kutoa fedha kwaajili ya miradi isiyo jihusisha na masuala ya dawa za kupunguza maumivu, na kuhamasisha matumizi ya dawa za kuondoa maumivu zisizo na madhara.
Na ni jambo lililo ndani ya uwezo wetu.Lakini pia tunatoa ushauri,na idara yetu ya inaliangalia suala hili kwa makini ikiwemo kuchukua hatua za kisheria,na tutalisimamia katika hatua ya kiserikali''
Rais Trump ameahidi kujenga taifa huru katika masuala ya matumizi ya dawa za kulevya kwa kizazi kijacho na kuhakikisha hakuna mazingira yatakayosababisha watu kujitumbukiza katika matumizi ya kulevya.
No comments:
Post a Comment