Askofu mkuu wa Cantebury ,Justin Welby anawatembelea viongozi wa
kisiasa pamoja na wale wa kidini nchini Misri ili kuzungumzia kuhusu
mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya wakristo katika eneo la mashariki
ya kati.
Askofu huyo ambaye ndio kiongozi wa Kanisa la Anglikana anatarajiwa kukutana na rais wa Misri Abdul Fattah al Sisi.
Pia
atatoa rambirambi zake kwa wakristo wa kanisa la Coptic ambao
walitekwanyara na kuuawa na wanamgambo wa Islamic State nchini Libya
mnamo mwezi wa Februari.
Askofu huyo amesema kuwa utekajinyara wa wakristo katika eneo hilo ni m'baya zaidi kwa karne kadhaa.
Pia
atakutana na Imam mkuu wa chuo cha al-Azhar ambacho ndio taasisi kuu
nchini Misri na inaheshimiwa na waislamu wa Sunni kama taasisi kubwa
zaidi ya mafunzo ya kiislamu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.