Waziri Mkuu Mizengo
Pinda amesema kuwa siyo jambo baya kwake kutajwa kutaka kuwania urais
katika uchaguzi mkuu ujao 2015 na kwamba kujitokeza pia ni jambo jema.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti
hili nyumbani kwake mjini Dodoma juzi, ambapo alizungumzia mambo
mbalimbali, Pinda alisema kuwa jambo la msingi kwa wote wenye nia ya
kuwania nafasi hiyo ya juu ya uongozi nchini ni kutambua kuwa urais ni
dhamana kutoka kwa wananchi na haupatikani kwa uamuzi wa anayegombea,
bali taratibu za vyama na wananchi watakaopiga kura.
Pinda maarufu kama Mtoto wa Mkulima alisema pia
kwamba ni muhimu kwa watu wanaotaka kuwania urais wasikiuke misingi ya
haki kwa kuingilia mchakato na kuwadhoofisha watu wenye mamlaka ya
kuchagua mgombea urais, bali waachwe ili wafanye uamuzi wa haki kwa
manufaa ya taifa, huku akisisitiza kufuatwa kwa taratibu za Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
“Kujitokeza ni jambo jema, kutajwatajwa nako pia
ni jambo jema tu kwa maoni yangu. Ninachoweza kusema kikubwa, wote
wanaotaka kwenda kwenye hiyo nafasi, rai yangu kubwa ni moja tu,
watambue wanachotaka kwenda kufanya ni dhamana. Ni nafasi kubwa, lakini
ni dhamana tu unapewa kwa niaba ya Watanzania wengine wote.Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz