Tuesday, March 20, 2018

TRUMP APENDEKEZA ADHABU YA KIFO KWA WAUZA MADAWA YA KULEVYA

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa anataka kuweka adhabu kali ikiwemo adhabu ya kifo kwa wale watakaobaninika kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya. Hatua amesema ni kwa lengo la kukabiliana na ongezeko kubwa watumiaji ndani ya Marekani.
Katika hotuba yake aliyoitoa akiwa New Hampshire,wauzaji wa dawa za kulevya wamesababisha vifo vya maelfu ya watu, lakini cha ajabu baada ya kuhukumiwa kufungwa wanakaa muda mfupi tu gerezani jambo ambalo anasema haliridhishwi nalo.
Ameongeza kuwa tatizo hili linaweza kuondolewa kwa kutumia akili na kuwa imara pamoja na kutenga fedha.
"Mwezi oktoba tulitangaza tatizo hili kama janga la dharula kiafya ambalo limedumu kwa muda mrefu tangu kipindi kilichopita.Tumelifanyia kazi na bunge kuhakikisha tunatenga kiasi cha dola billion sita katika bajeti mpya yam waka 2018/2019 ili kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya,ambapo tutakuwa tumetenga kiasi kikubwa cha fedha kuwahi kutokea dhidi ya tatizo hili'.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MARCH 20, 2018 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


Tunapenda kuwataarifu wadau wa Jambo Tz kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz

Monday, March 19, 2018

PICHA ZA RAIS MAGUFULI AKIENDESHA MKUTANO WA 11 WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 
 Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018

 Sehemu ya Viongozi wa serikali na wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Viongozi wa wa taasisi mbali mbali katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Ujumbe wa Umoja wa nchi za Ulaya (EU) katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018. Tunapenda kuwataarifu wadau wa blog ya Jambo Tz kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz

Saturday, February 4, 2017

TAZAMA PICHA 30 BORA ZA OBAMA KATI YA MILLION 2 ALIZOPIGWA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA NANE


Pete Souza katika kipindi cha miaka 8 amempiga picha zaidi ya million 2 rais mstaafu wa Marekani. Pete ambae alikuwa mpiga picha wa familia ya Obama aliambatana nae rais huyo kwa kipindi chote cha miaka nane ya uongozi wake.
 
Tu-follow instagram@jambotz. Like page yetu ya facebook ya Jambo Tz.

Wednesday, January 25, 2017

ECOWAS WABAINI KEMIKALI YA SUMU IKULU YA GAMBIA

Rais mstaafu wa Gambia Yahya Jammeh

Askari wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (Ecowas) wamegundua kemikali ya sumu kali iliyokuwa imetegwa kwenye vyumba vya Ikulu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Ecowas kupitia gazeti la Freedom la Gambia, kemikali hiyo ilitegwa kwa lengo la kuua mtu yeyote atakayeingia ndani ya Ikulu hiyo.

Kutokana na hali hiyo, kiongozi mpya wa Gambia, Adama Barrow anatakiwa kuendelea kukaa Senegal kwa usalama wake huku uchunguzi ukiendelea kufanyika.

Sunday, January 1, 2017

KHERI YA MWAKA MPYA 2017

Uongozi wa Keny Pino Blog unawatakia kheri ya mwaka mpya 2017 na fanaka tele, Mwenyezi Mungu awabariki na kuwalinda siku zote. HAPPY NEW YEAR.


Thursday, May 5, 2016

HUKUMU KESI YA KAFULILA MEI 17

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora inayosikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Kigoma Kusini iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila inatarajia kutoa hukumu Mei 17, mwaka huu.

Jaji wa mahakama hiyo anayesikiliza kesi hiyo mjini Kigoma, Ferdinand Wambali, alisema kuwa amepanga kutoa hukumu tarehe hiyo baada ya pande zote mbili kuwasilisha ushahidi na maelezo yao.

Baada ya kukamilika kwa ushahidi huo, Jaji Wambari aliomba kupatiwa muda wa kutosha kupitia ushahidi na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo ili aweze kutoa hukumu ya haki.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza, Ruben Mfune ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo ni mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyo. Katika kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2015, Kafulila anaishawishi mahakama itengue matokeo yaliyompa ushindi aliyekuwa mgombea wa CCM, Hasna Mwilima badala yake imtangaze yeye kama mshindi halali wa jimbo hilo.

Walalamikiwa katika kesi hiyo ni pamoja na Mbunge wa jimbo hilo Hasna, aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza, Ruben Mfune ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo na Mwanasheria wa Serikali ambaye anaiwakilisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Katika kesi hiyo, Wakili Kenedy Fungamtama anamtetea Husna huku Kafulila akitetewa na mawakili watatu, Profesa Abdallah Safari, Tundu Lissu na Daniel Rumenyela.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS MEI 05, 2016 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

20160505_074606 20160505_074619 20160505_074634 20160505_074644 20160505_074726

VYUO VIKUU BORA DUNIA

Orodha mpya ya vyuo vikuu bora zaidi duniani ya Times Higher Education, kwa kuangazia sifa za chuo kikuu husika, imetolewa, huku vyuo vikuu kutoka bara Asia vikiimarika sana. Mwaka huu, kuna vyuo vikuu 17 kutoka Asia vilivyomo kwenye orodha ya vyuo 100 bora, likiwa ongezeko kutoka vyuo 10 mwaka jana.

Kwa mara ya kwanza, kuna chuo kikuu kutoka Uchina katika 20 bora, Chuo Kikuu cha Tsinghua University kutoka Beijing ambacho kimo nambari 18. Vyuo vikuu vya Marekani bado vinatawala orodha hiyo, chuo kikuu cha Harvard kikiwa ndicho kinachoongoza. Vifuatavyo ni vyuo vikuu bora 100.

1 . Harvard University

Marekani

2 . Massachusetts Institute of Technology

Marekani

3. Stanford University

Marekani

WAPENZI WA JINSIA MOJA WAPINGA UKAGUZI WA 'TUPU ZA NYUMA'

wapenzi wa jinsia moja
 
Wanaume wawili wanaosema kuwa maafisa wa polisi wa Kenya waliwalazimisha kufanyiwa ukaguzi wa tupu ya nyuma ili kubaini kwamba walishiriki katika ngono ya mapenzi ya jinsia moja wameanzisha kesi mahakamani wakitaka ukaguzi huo kuwa ukiukaji wa katiba.

Wanasema kuwa walilazimishwa kufanyiwa ukaguzi wa magonjwa ya virusi vya ukimwi na Hepatitis kufuatia kukamatwa kwao mnamo mwezi Februari 2015 baada ya kushukiwa kwamba wanashiriki katika ngono ya mapenzi ya jinsia moja.

Vitendo vya wapenzi wa jinsia moja kushiriki ngono ni kinyume na sheria nchini Kenya na adhabu ya makosa hayo ni miaka 14 jela. Mahakama ya Mombasa imewapatia mawakili wa serikali wiki moja kutoa jibu. Chini ya sheria ya kimataifa, ukaguzi wa lazima katika tupu ya nyuma ni kitendo cha kikatili,unyama na ni sawa na mateso kulingana na kundi la haki za kibinaadamu Human Wrights Watch.

KATUMBI ATANGAZA KUWANIA URAIS CONGO

 Mwanasiasa mashuhuri nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Moise Katumbi amethibitisha kuwa atagombea urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba.

Mfanyabiashara huyo na gavana wa zamani wa jimbo la Katanga alitoa tangazo hilo kupitia kwa mitandao ya kijamii. Muungano wa vyama kadha vya upinzani uliamua kumuidhinisha Bw Katumbi kuwa mgombea mwezi Machi.
Bw Katumbi, akitangaza kuwania kwake, amepuuzilia mbali madai kwamba alipokuwa waziri wa hati alitumia mamluki kutoka nje akisema habari hizo ni za uongo. Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo Rais Joseph Kabila anatakiwa kuondoka madarakani mwaka huu lakini wapinzani wake wana hofu kuwa huenda ana mipango ya kusalia madarakani.

CHURA AMPONZA 'SNURA MAJANGA' AFUNGIWA KUFANYA KAZI ZA SANAA

SERIKALI imesitisha wimbo na video ya ‘Chura’ wa msanii, Snura Mushi ‘Snura Majanga’, kuchezwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari hadi itakapofanyiwa marekebisho. Wimbo na video hiyo umetokana na maudhui ya utengenezwaji wake ambayo hayaendani na maadili ya Mtanzania.
Pia Serikali imesitisha maonyesho yote ya hadhara ya msanii huyo, mpaka atakapokamilisha taratibu za usajili wa kazi zake za sanaa katika Baraza la Sanaa la Taifa (Basata). Licha ya hivyo, Serikali imewataka wasanii wajiulize kabla ya kubuni kazi zao za sanaa kwa kufikiria wazazi, ndugu, jamaa na marafiki zao namna watakavyozipokea.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano serikalini, Zawadi Msalla, aliwaambia waandishi wa habari kwamba wasanii wanapotunga nyimbo zao wavae nafasi za wanaowadhalilisha na waelewe kwamba sanaa si uwanja wa kudhalilisha watu.

MAN CITY WACHAPWA 1-0 NA REAL MADRID

 
Manchester City wameshindwa kufika katika fainali za kwanza za klabu bingwa barani Ulaya (UEFA) baada ya kutolewa na mabingwa mara 10 wa michuano hiyo Real Madrid katika mchezo uliokua wa kuvutia tena wa aina yake. Walichapwa 1-0.

Baada ya kutokuwa na ushindi wowote katika mzunguko wa kwanza, Real Madrid walianza kuongoza kipindi cha kwanza kufuatia mpira wa krosi uliopigwa na Gareth Bale kumbabatiza kiungo wa City Fernando na kuingia nyavuni.
Real waliutawala mchezo huku mpira wa kichwa uliopigwa na Bale ukigonga mwamba na baadaye mlinda mlango wa City Joe Hart akiondoa mikwaju ya Luka Modric na Cristiano Ronaldo. 

Klabu hiyo ya Uingereza ilikuwa ikihitaji bao moja muhimu la ugenini hususan katika dakika za lala salama kuelekea fainali,lakini hilo halikuweza kufanikiwa licha ya kushangiliwa na mashabiki wake wapatao 4,500.

Madrid walipata wakati mgumu kidogo pale mkwaju mkali wa Sergio Aguero ulipogonga nyavu za juu za lango la Madrid. Real sasa watakutana na Atletico katika uwanja wa San Siro tar 28 Mei, hii ikiwa ni kama marudio ya fainali za mwaka 2014 ambapo Real walishinda kwa mabao 4-1 baada ya muda wa nyongeza.

Tuesday, April 19, 2016

MAGUFULI ATINGA CRDB KAMA RAIA WA KAWAIDA...!!!

Rais John Pombe Magufuli akiondoka katika benki ya CRDB, Tawi la Holland baada ya kumaliza shughuli iliyompeleka.

Rais John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi mkono wakati akiondoka katika benki ya CRDB, Tawi la Holland. 

Wakati akikaribia kuingia ndani ilibidi baadhi ya wateja waliyokuwa wakijiandaa kuingia ndani ya benki hiyoi wazuiwe kuingia huku huduma ikiendelea tu kwa wale ambao waliyokwishaingia. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.
Aidha, baada ya kuingia ndani baadhi ya wateja wa tawi hilo na wananchi wengine walibaki wakishangaa huku wengine wakijiuliza imekuwaje Rais kuingia benki kwa sitaili ile. Baadhi ya wananchi walisema hawajaona tukio kama lile kwa Marais wote waliyopita.

James Charles, ambaye ni dereva wa taxi, alisema baadhi ya wananchi waliyokuwa kwenye eneo hilo baada ya kuona ulinzi unaimarishwa walishituka na mara wakamuona Rais Magufuli akishuka kwenye gari, hali iliyowafanya wafikirie anakwenda kutembelea ofisi yake ya zamani.

“Lakini kufumba na kufumbua tukamuona anaelekea kwenye benki ya CRDB, tukajiuliza vipi rais leo kaamua kuwa kama mteja? Hata hivyo tujui kama hiyo ilikuwa inawezekana. Lazima kutakuwa na kitu. Haiwezekani aende akachukue fedha kwa utaratibu ule. Ngoja tusubiri tutasikia amefuata nini,” alisema Charles.

Joyce Godwin ambaye ni mwanafunzi wa chuo kimojawapo cha elimu ya juu alisema kuja kwake kumewashtua wafanyakazi wa tawi la benki hiyo kwani walidhani alikwenda pale kwa ajili ya kutumbua majipu.

“Mimi wakati Rais Magufuli anaingia nilikuwepo ndani kwenye foleni nikisubiri huduma. Kwa ujumla kila mmoja wetu alishituka lakini hatukujua kilichomleta,” alisema. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

MAAJABU: VIETJET AIR NDEGE AMBAYO WAHUDUMU WAKE HUVAA BIKINI...!!!

icghfhec

iegfehbi

jahjhcbj 

Kampuni ya Ndege ya VietJet Air ya nchini Vietnam imejizolea umaarufu mkubwa nchini humo kutokana na kutoa huduma kwa watalii kwa mfumo wa tofauti na makampuni mengine nchini humo. Huduma ambazo zinatolewa katika ndege hiyo ni pamoja na wahudumu wa ndege kuvaa bikini pindi wanapokuwa wanawahudumia watalii wanapokuwa safarini kuwapeleka sehemu ya kitalii Nha Trang. 
   
Licha ya Mamlaka ya Anga ya Vietnam kuwapiga faini ya Dola 960 ( Mil. 2.1kwa pesa ya Kitanzania) kwa wahudumu wao kuvaa bikini bila ya kuwa na kibali lakini bado wameendelea kutoa huduma kwa mfumo huo na kuwafanya kuzidi kujizolea umaarufu mkubwa na kujiingizia faida zaidi. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...