Thursday, May 5, 2016

HUKUMU KESI YA KAFULILA MEI 17

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora inayosikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Kigoma Kusini iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila inatarajia kutoa hukumu Mei 17, mwaka huu.

Jaji wa mahakama hiyo anayesikiliza kesi hiyo mjini Kigoma, Ferdinand Wambali, alisema kuwa amepanga kutoa hukumu tarehe hiyo baada ya pande zote mbili kuwasilisha ushahidi na maelezo yao.

Baada ya kukamilika kwa ushahidi huo, Jaji Wambari aliomba kupatiwa muda wa kutosha kupitia ushahidi na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo ili aweze kutoa hukumu ya haki.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza, Ruben Mfune ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo ni mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyo. Katika kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2015, Kafulila anaishawishi mahakama itengue matokeo yaliyompa ushindi aliyekuwa mgombea wa CCM, Hasna Mwilima badala yake imtangaze yeye kama mshindi halali wa jimbo hilo.

Walalamikiwa katika kesi hiyo ni pamoja na Mbunge wa jimbo hilo Hasna, aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza, Ruben Mfune ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo na Mwanasheria wa Serikali ambaye anaiwakilisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Katika kesi hiyo, Wakili Kenedy Fungamtama anamtetea Husna huku Kafulila akitetewa na mawakili watatu, Profesa Abdallah Safari, Tundu Lissu na Daniel Rumenyela.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS MEI 05, 2016 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

20160505_074606 20160505_074619 20160505_074634 20160505_074644 20160505_074726

VYUO VIKUU BORA DUNIA

Orodha mpya ya vyuo vikuu bora zaidi duniani ya Times Higher Education, kwa kuangazia sifa za chuo kikuu husika, imetolewa, huku vyuo vikuu kutoka bara Asia vikiimarika sana. Mwaka huu, kuna vyuo vikuu 17 kutoka Asia vilivyomo kwenye orodha ya vyuo 100 bora, likiwa ongezeko kutoka vyuo 10 mwaka jana.

Kwa mara ya kwanza, kuna chuo kikuu kutoka Uchina katika 20 bora, Chuo Kikuu cha Tsinghua University kutoka Beijing ambacho kimo nambari 18. Vyuo vikuu vya Marekani bado vinatawala orodha hiyo, chuo kikuu cha Harvard kikiwa ndicho kinachoongoza. Vifuatavyo ni vyuo vikuu bora 100.

1 . Harvard University

Marekani

2 . Massachusetts Institute of Technology

Marekani

3. Stanford University

Marekani

WAPENZI WA JINSIA MOJA WAPINGA UKAGUZI WA 'TUPU ZA NYUMA'

wapenzi wa jinsia moja
 
Wanaume wawili wanaosema kuwa maafisa wa polisi wa Kenya waliwalazimisha kufanyiwa ukaguzi wa tupu ya nyuma ili kubaini kwamba walishiriki katika ngono ya mapenzi ya jinsia moja wameanzisha kesi mahakamani wakitaka ukaguzi huo kuwa ukiukaji wa katiba.

Wanasema kuwa walilazimishwa kufanyiwa ukaguzi wa magonjwa ya virusi vya ukimwi na Hepatitis kufuatia kukamatwa kwao mnamo mwezi Februari 2015 baada ya kushukiwa kwamba wanashiriki katika ngono ya mapenzi ya jinsia moja.

Vitendo vya wapenzi wa jinsia moja kushiriki ngono ni kinyume na sheria nchini Kenya na adhabu ya makosa hayo ni miaka 14 jela. Mahakama ya Mombasa imewapatia mawakili wa serikali wiki moja kutoa jibu. Chini ya sheria ya kimataifa, ukaguzi wa lazima katika tupu ya nyuma ni kitendo cha kikatili,unyama na ni sawa na mateso kulingana na kundi la haki za kibinaadamu Human Wrights Watch.

KATUMBI ATANGAZA KUWANIA URAIS CONGO

 Mwanasiasa mashuhuri nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Moise Katumbi amethibitisha kuwa atagombea urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba.

Mfanyabiashara huyo na gavana wa zamani wa jimbo la Katanga alitoa tangazo hilo kupitia kwa mitandao ya kijamii. Muungano wa vyama kadha vya upinzani uliamua kumuidhinisha Bw Katumbi kuwa mgombea mwezi Machi.
Bw Katumbi, akitangaza kuwania kwake, amepuuzilia mbali madai kwamba alipokuwa waziri wa hati alitumia mamluki kutoka nje akisema habari hizo ni za uongo. Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo Rais Joseph Kabila anatakiwa kuondoka madarakani mwaka huu lakini wapinzani wake wana hofu kuwa huenda ana mipango ya kusalia madarakani.

CHURA AMPONZA 'SNURA MAJANGA' AFUNGIWA KUFANYA KAZI ZA SANAA

SERIKALI imesitisha wimbo na video ya ‘Chura’ wa msanii, Snura Mushi ‘Snura Majanga’, kuchezwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari hadi itakapofanyiwa marekebisho. Wimbo na video hiyo umetokana na maudhui ya utengenezwaji wake ambayo hayaendani na maadili ya Mtanzania.
Pia Serikali imesitisha maonyesho yote ya hadhara ya msanii huyo, mpaka atakapokamilisha taratibu za usajili wa kazi zake za sanaa katika Baraza la Sanaa la Taifa (Basata). Licha ya hivyo, Serikali imewataka wasanii wajiulize kabla ya kubuni kazi zao za sanaa kwa kufikiria wazazi, ndugu, jamaa na marafiki zao namna watakavyozipokea.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano serikalini, Zawadi Msalla, aliwaambia waandishi wa habari kwamba wasanii wanapotunga nyimbo zao wavae nafasi za wanaowadhalilisha na waelewe kwamba sanaa si uwanja wa kudhalilisha watu.

MAN CITY WACHAPWA 1-0 NA REAL MADRID

 
Manchester City wameshindwa kufika katika fainali za kwanza za klabu bingwa barani Ulaya (UEFA) baada ya kutolewa na mabingwa mara 10 wa michuano hiyo Real Madrid katika mchezo uliokua wa kuvutia tena wa aina yake. Walichapwa 1-0.

Baada ya kutokuwa na ushindi wowote katika mzunguko wa kwanza, Real Madrid walianza kuongoza kipindi cha kwanza kufuatia mpira wa krosi uliopigwa na Gareth Bale kumbabatiza kiungo wa City Fernando na kuingia nyavuni.
Real waliutawala mchezo huku mpira wa kichwa uliopigwa na Bale ukigonga mwamba na baadaye mlinda mlango wa City Joe Hart akiondoa mikwaju ya Luka Modric na Cristiano Ronaldo. 

Klabu hiyo ya Uingereza ilikuwa ikihitaji bao moja muhimu la ugenini hususan katika dakika za lala salama kuelekea fainali,lakini hilo halikuweza kufanikiwa licha ya kushangiliwa na mashabiki wake wapatao 4,500.

Madrid walipata wakati mgumu kidogo pale mkwaju mkali wa Sergio Aguero ulipogonga nyavu za juu za lango la Madrid. Real sasa watakutana na Atletico katika uwanja wa San Siro tar 28 Mei, hii ikiwa ni kama marudio ya fainali za mwaka 2014 ambapo Real walishinda kwa mabao 4-1 baada ya muda wa nyongeza.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...