Baada
ya vyombo vya habari kuripoti kuhusu Waziri wa Maliasili na Utalii
Lazaro Nyalandu(Pichani juu) na msanii wa filamu Aunty Ezekiel kuvinjari
nchini Marekani hatimaye waziri huyo
Aunt Ezekiel
alisema tuhuma hizo zimetengenezwa na kundi la watu ambalo miongoni mwao
ni baadhi ya viongozi wa Serikali ambao humchafua kutokana na utendaji
kazi wake.
Nyalandu alisema alikwenda Marekani septemba12 kwa ajili ya kufungua
tamasha la utamaduni na utalii kupitia soko la wasanii wa Tanzania
ambako alikutana na msanii huyo mara moja pamoja na mwingine wa Bongo
Fleva Kassim Mganga usiku katika moja ya maeneo nchini humo.
Alikana kutanua na msanii huyo kama baadhi ya nyombo vya habari
vilivyoripoti na kusema maneno hayo ni kwa lengo la kumwaribia heshima
yake mbele ya jamii. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz