Wednesday, November 19, 2014

WAPINZANI WAMSULUBU MWAKYEMBE BUNGENI



Dk Harrison Mwakyembe
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, jana ilimsulubu Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ikieleza kuwa wizara yake iliingia mkataba wa mradi wa treni za kisasa kutoka Stesheni ya Dar es Salaam hadi Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) bila kufuata taratibu.
Kambi hiyo ililieleza Bunge kuwa mkataba huo ulisainiwa baina ya mmiliki wa Kampuni ya M/s Shumoja, Robert Shumake na Shirika la Reli Tanzania huku Waziri Mwakyembe akishuhudia.
Msemaji Mkuu wa kambi hiyo, Ofisi ya Waziri Mkuu,  Uwekezaji na Uwezeshaji, Pauline Gekul alitoa madai hayo wakati akiwasilisha maoni ya kambi hiyo kuhusu muswada wa marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP). Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

NABII: "URAIS 2015 BALAA!... JK ASINGEWAHI KUPASULIWA, NCHI INGECHAFUKA"




NABII wa Kanisa la The Revelation lililopo Buza Kipera jijini Dar, Yaspi Bendera amesema uchaguzi mkuu ujao utakuwa balaa kubwa kufuatia maono anayoyaona wakati akishiriki ibada katika nyakati mbalimbali, Risasi Jumatano linakupa mkanda kamili.

Nbii wa Kanisa la The Revelation lililopo Buza Kipera jijini Dar, Yaspi Bendera.

Akizungumza wakati wa ibada kanisani kwake na baadaye na waandishi wetu Novemba 16 mwaka huu, Nabii Yaspi alisema kuna mgongano mkubwa miongoni mwa watu wanaotajwa kugombea urais, ili kumrithi rais Jakaya Kikwete ambaye alimwelezea kama kiongozi anayemuona kiroho kila mara.


“Nilimuona katika maono yangu kama mtu aliye kwenye majaribu makubwa kiroho, nikaandaa maombi hapa kanisani na tukamuombea kwa muda wa nusu saa na tunashukuru Mungu hali yake inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi dume nchini Marekani. Bado namuona akiwa na maumivu kuanzia sehemu za kiuno, uti wa mgongo na shingoni mwake.

Mhe. Edward Lowasa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

UJERUMANI YAIUA HISPANIA 1-0

Mario Gotze, who scored Germany's winning goal at the World Cup final, is put under pressure by Cesar Azpiliciueta and Sergio Busquets 
Mario Gotze akiwapita Cesar Azpiliciueta wa Sergio Busquets wa Hispania katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa mjini Vigo. Ujerumani ilishinda 1-0, bao pekee la Toni Kroos dakika ya mwisho.
Gotze is grounded under the challenge of Spain defender Sergio Ramos as the rain beings to fall in Vigo on Tuesday evening
Gotze akienda chini baada ya kukwatuliwa na beki wa Hispania, Sergio Ramos. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Monday, November 3, 2014

MAGAZETI YA LEO JUMATATU NOVEMBA 03, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WARIOBA ADHALILISHWA KATIKA MDAHARO WA KATIBA...!!!

Waziri Mkuu mstaafu Joseph Warioba akisaidiwa kutolewa katika vurugu
Katika mazingira ya kutatanisha, jana Jumapili Novemba 02, mwaka huu vurugu zimekatisha mdahalo uliokuwa ukiendelea kujadili mchakato wa katiba mpya ya Tanzania huku baadhi ya watu wakipigwa na kujeruhiwa.
Mdahalo huo uliokuwa ukitangazwa moja kwa moja kupitia redio na televisheni za hapa nchini  ulivurugika kutokana na kundi la vijana wapatao 20 kuanza kumzomea aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, alipokuwa akiwasilisha mada yake.
Vijana hao ambao haijajulikana walitokea wapi au walikuwa na ajenda gani waliinua mabango ya kupinga msimamo wa waliokuwa wakiendesha mdahalo na kusema rasimu ya katiba iliyopendekezwa inakidhi mahitaji yote na kusema hakuna haja ya mdahalo.
Jaji Warioba ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania alifanikiwa kutoka salama nje ya ukumbi ulipokuwa ukifanyika mdahalo huo jijini Dar Es Salaam, lakini wapo watu waliojeruhiwa kutokana na kurushwa viti na vitu vingine. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAANDAMANO ZAIDI YAFANYWA BURKINA FASO



Jeshi la Burkina Faso limefyatua risasi hewani kuwatawanya waandamanaji nje ya kituo cha utangazaji cha taifa katika mji mkuu, Ouagadougou.
Ripoti zinasema kuwa risasi zilifyatuliwa punde baada ya kiongozi wa upinzani, Sara Sereme, kuwasili pamoja na wafuasi wake.
Wanajeshi waliwatawanya maelfu ya waandamanaji waliokusanyika katika medani kuu mjini Ouagadougou.
Vyama vya upinzani vinataka iwekwe serikali ya muda ya raia hadi uchaguzi wa rais utapofanywa.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa mjini humo, Mohamed ibn Chambas, ameonya kuwa Burkina Faso inaweza kuwekewa vikwazo iwapo jeshi litaendelea kuongoza nchi. Asante kwa kutembelea blog hii, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MSIMAMO WA VODACOM PREMIER LEAGUE (VPL) KWA SASA

 
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...